Afisa Mtendaji Mkuu wa klanu ya Simba Bw. Crecentius Magori akizungumza na waandishi wa habari kuhusu maandakizi ya matukio mbalimbali ya wiki ya Tamasha la Simba ambalo litafanyika Agosti 6 mwaka huu kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam, Mkutano huo umefanyika kwenye hoteli ya Serena jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Sports Pesa Tarimba Abas akizungumza na waandishi wa habari katika mkutano huo kama mdhamini wa klabu hiyo.
Msemaji wa Klabu ya Simba Bw. Haji Manara akiwatambulisha viongozi wa Simba na mdhamini wa timu hiyo Sports Pesa kwa ajili ya kuzungumzaam.a na waandishi wa habari kwenye hoteli ya Serena jijini Dar es sal
Waandishi wa habari mbalimbali wakimsikiliza Mtendaji Mkuu wa Simba Bw. Crecentius Magoro wakati akizungumza nao kwenye hoteli ya Serena jijini Dar es salaam.
………………………………………………………….
UONGOZI wa Klabu ya Simba wametoa ratiba ya tamasha la Simba Day ambalo wanatarajia kuanza Julai 31 mwaka huu hadi Julai 6 ambayo ndio siku ya kilele.
Akizungumza kuhusu tamasha la Simba Day, Mkurugenzi Mtendaji wa Klabu ya Simba …amesema kwa kujibu wa mkataba wa tamasha hilo kwa mwaka huu litafahamika kwa Sportpesa Simba Week na hiyo ni kwa kujibu wa mkataba.
Amesema katika wiki ya tamasha hilo kutakuwa na ratiba ya shughuli ambazo zitafanyika yakiwemo matukio ya kusaidia jamii ya Watanzania na hivyo ameshauri utaratibu huo utafanyika kwa Wana Simba kote nchini.
Akizungumzia ratiba ya tamasha hilo wataanza Julai 31 ambayo itakuwa Jumatano na siku hiyo wachezaji wa klabu hiyo watarejea nchini wakitoa Afrika Kusini ambako walikuwa wameweza kambi.
Wachezaji waliopo kambini watakuja nchini wakitoka Afrika tisini. ambapo Pia siku hiyo watasaini makubaliano ya mkataba wa jezi na vifaa vya mazoezi na mdhamini wa klabu hiyo kampuni ya Romario 2000.
Mkataba huu ni wa miaka miwili na siku hiyo wataeleza kwa undani kuhusu mkataba.
Siku ya tarehe moja Watanzania wawe kwenye mitandao kwani ndiyo siku ambayo jenzi hizo zitazinduliwa kwa ajili ya msimu mpya wa ligi kuu ya TPL wa mwaka 2019/2020.
Jezi za ugenini, ni nyekundu za nyumbani ni Nyeupe na nnatural ni pale timu zinapokutana jenzi zikiwa zinafanana ndipo zinatumika hizo. mara baada ya uzinduzi huo jezi za simba zitaanza kuzwa nchi nzima , na utaratibu wa kuuza jezi utaelezwa hapo baadaye.