Home Mchanganyiko CEED TANZANIA YATOA MAFUNZO YA KUKUZA NA KUSIMAMIA BIASHARA KWA WAJASIRIAMALI NCHINI.

CEED TANZANIA YATOA MAFUNZO YA KUKUZA NA KUSIMAMIA BIASHARA KWA WAJASIRIAMALI NCHINI.

0
Mwakilishi kutoka CEED Bw. Fred Laiser akiongea na wanahabari (hawapo pichani)
 

Bi. Elizabeth Swai mjasiliamali wa biashara ya kuku akichangia moja ya mada.
 

Bw. Robin Zimbakov kutokea nchini Macedonia akichangia moja ya mada.
 
Baadhi ya Wajasiriamali waliohudhuria
 
Kituo cha Ujasiriamali na Maendeleo ya Utendaji (CEED), yawakutanisha wafanyabiashara mbalimbali wa mazao ya kilimo na usindikizaji vyakula katika hafla iliyolenga kutoa mafunzo ya usimamizi, maarifa ya biashara, utayari wa uwekezaji na fursa za mtandao.
 
Akizungumza na waandishi wa habari,mwakilishi kutoka CEED bwana Fred Laiser amesema lengo la hafla hii ni kutoa elimu kuhusu usimamizi wa biashara zao na kuwakutanisha wajasirimali kutoka ndani na nje ya nchi ili kujifunza mengi zaidi.
 
“Sisi CEED kazi yetu ni kuwainua wajasiriamali mbali mbali nchini hasa wa mazao ya kilimo pamoja na mifugo.Leo tupo hapa kwa ajili ya kuwapa elimu ya usimamizi wa biashara zao hasa zinapokuwa kubwa kwasababu biashara inapokuwa kubwa changamoto nazo zinaongezeka”,Alisema Fred.
 
Kwa upande wa washiriki kutoka Tanzania, Bi Elizabeth Swai mjasiliamali wa biashara ya kuku amesema amefurahia kupata mafunzo kutoka kwa wakufunzi wa kimataifa ambayo yatamuwezesha kuendeleza biashara yake.
 
“Kuwa mjasiriamali kuna changamoto mbalimbali, hasa kipindi ambacho biashara yako inakua changamoto zinakuwa ngumu zaidi. Kama mjasiriamali ni muhimu sana kujibadilisha kila wakati ili kutoa huduma bora au bidhaa bora kushindina katika soko”. Elizabeth Swai.
 
Hafla hiyo imeudhuriwa na wafanyabiashara takribani 40 kutoka kona mbalimbali kutoka ndani na nje Tanzania akiwemo mfanyabishara wa kimataifa mwenye mafanikio makubwa bwana Robin Zimbakov ambaye aliezea safari yake ya ujasirimali, changamoto alizokutanazo hadi biashara yake kusimama.