Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge Uratibu na wenye Ulemavu Profesa Palamaganda Kabudi ameendelea na ziara yake katika Mkoa wa Dar es Salaam ambapo ametembelea ujenzi wa barabara ya kilongawima iliyopo wilaya Kinondoni, amezindua jengo la mama na mtoto Hospitali ya vijibweni iliyopo wilaya ya Kigamboni pamoja na kukagua ujenzi wa shule ya Sekondari Kibondemajaji na shule ya msingi Vigoa zilizopo Wilaya ya Temeke

Akizungumza wakati akikagua ujenzi wa barabara ya kilongawima Kinondoni jijini Dar es Salaam inayojengwa na mkandarasi mzawa Kings builders, Profesa Kabudi pamoja na kuridhishwa na ujenzi huo amewataka wakandarasi wazawa kuwa wazalendo kwenye kazi kwani Rais Dokta Samia ameelekeza wazawa wapewe miradi ya ujenzi na hiyo sio hisani bali anatambua uwezo wao.

Aidha wakati akizindua jengo la mama na mtoto Hospitali ya vijibweni wilaya ya Kigamboni Profesa Kabudi amesema moja ya mambo ambayo Rais Dokta Samia ameyapa kipaumbele ni suala la mama na mtoto jambo lililopelekea heshima ya kuwa kinara wa Afya ya mama na mtoto katika bara la Afrika Tanzanzania imekua ni kimbilio la huduma za afya ikiwemo za figo na moyo

Akiwa katika miradi ya ujenzi wa shule ya msingi Vigoa na shule ya Sekondari Kibondemaji amezungumzia maboresho ya mfumo wa elimu ambapo elimu ua msingi inaishia kidato cha nne ma kwamba shule za msingi wanafunzi wanaishia darasa la sita kuanzia mwaka 2027

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Dar es sallm Mhe Albert Chalamila alipozungumza kwenye mradi wa ujenzi wa barabara ya kilongawima amezungumzia suala la wakandarasi wazawa ambao kwa sasa wamekua wakipewa kipaumbele na akiwa kwenye mradi wa jengo la mama na mtoto amehimiza nidhamu ya fedha kwenye ujenzi

Emanuel Atanas Mkuchu ni Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa wa kilongawima ameeleza changamoto zilizokuwa zikiwakabili wananchi kutokana na ubovu wa barabara hiyo na kuomba Serikali kujenga barabara zingine kwenye eneo hilo ili kumaliza changamoto ya usafiri