Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, akiwa kwenye mazungumzo na Rais wa Jamhuri ya Ghana, Mhe. John Dramani Mahama, katika Ikulu ya nchi hiyo Jubilee House, jijini Accra, Ghana, tarehe 22 Julai, 2026. Pamoja na mambo mengine, Rais Mhe. Dkt. Samia na Mwenyeji wake Rais Mhe. Mahama walikubaliana kuimarisha ushirikiano kwa kutekeleza kwa pamoja masuala mbalimbali ya afya. Pia, walizungumzia ushirikiano na kubadilishana uzoefu kwenye sekta ya madini ambapo kwa upande wa Ghana asilimia 60 ya uzalishaji unafanywa na wachimbaji wadogo na asilimia 40 unafanywa na wachimbaji wakubwa, hali inayowanufaisha wananchi wa kawaida. Kuhusu Biashara baina ya nchi mbili kuwa na muamko mdogo, waligusia kuendelea kuipa msukumo mkubwa na hasa baada ya Shirikia la Ndege la Tanzania (Air Tanzania) kuanzisha safari katika ukanda huo wa Magharibi ambapo kumeanza kuchochea fursa mbalimbali za kiuchumi tofauti na awali.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan akiagana na Rais wa Jamhuri ya Ghana, Mhe. John Dramani Mahama, baada ya kuhitimisha Ziara yake ya kikazi katika Ikulu ya nchi hiyo Jubilee House, jijini Accra, Ghana, tarehe 22 Julai, 2026.
