Accra, Ghana — Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk Jakaya Mrisho Kikwete, amezitaka serikali za Afrika kuacha kutegemea zaidi matamko na ahadi zisizoambatana na utekelezaji, na badala yake kuweka fedha za ndani, uwajibikaji na matumiziya ubunifu kwa kiwango kikubwa kuwa msingi waajenda ya afya ya bara hilo.

Dk Kikwete ametoa wito huo katika Mjadala wa Ngazi ya Juu wa Sera ya Kukuza Agenda ya Afya Afrika, uliofanyika Jumatatu Julai 20, 2026 katika Hoteli ya Kempinski, Accra, pembezonimwa Mkutano Maalumu wa Umoja wa Afrika kuhusu Afya.

Mjadala huo uliwakutanisha mawaziri, watungasera, jumuiya za kiuchumi za kikanda, taasisi za bara, washirika wa maendeleo, viongozi wa sektabinafsi pamoja na wataalamu wa afya duniani.

Uliandaliwa kwa pamoja na African Renaissance Trust na Wakfu wa Jakaya Mrisho Kikwete, kwaushirikiano na Tume ya Umoja wa Afrika nawadau wengine, chini ya kaulimbiu: “KuendelezaAjenda ya Afya ya Afrika kupitia Ufadhili waNdani, Uwajibikaji na Ubunifu wa Kimkakati.”

Dk Kikwete alisema utegemezi wa muda mrefuwa Afrika kwa misaada ya nje katika kugharamiahuduma za afya hauwezi tena kuendelea kuwamsingi mkuu wa mifumo ya afya ya bara hilo.

Alisema kupungua kwa misaada ya maendeleo, kuongezeka kwa madeni ya serikali na mahitaji makubwa ya huduma bora za afya vinailazimisha Afrika kubadilisha namna inavyofadhili na kusimamia sekta hiyo.

“Ujumbe kutoka Eswatini hadi Accra ni mmoja: Afrika lazima izidi kugharamia, kuzalisha na kulinda mustakabali wake wa afya,” alisema.

Mkutano huo umefanyika miaka 25 baada ya Azimio la Abuja la mwaka 2001, ambalo lilizitaka nchi wanachama wa Umoja wa Afrika kutenga angalau asilimia 15 ya bajeti zao za kitaifa kwaajili ya afya.