Katika kuboresha utendaji kazi wa Serikali na kutokana na baadhi ya viongozi kustaafu kazi, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi na uhamisho wa Wakuu wa Wilaya, Makatibu Tawala wa Wilaya na Wakurugenzi Watendaji wa Halmashauri. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Dkt. Moses Kusiluka, uteuzi na uhamisho huo ni kama ifuatavyo.


