Timu ya Taifa ya Hispania imefanikiwa kutinga hatua ya nusu fainali ya Kombe la Dunia 2026 baada ya kuichapa Ubelgiji mabao 2-1 katika mchezo wa robo fainali.

Kwa matokeo hayo, Ubelgiji imeaga rasmi mashindano hayo, huku Hispania ikiendelea na safari ya kusaka ubingwa.

Katika hatua ya nusu fainali, Hispania itakutana na Ufaransa katika mchezo utakaopigwa Julai 14, 2026, saa 4:00 usiku, huku kila timu ikisaka tiketi ya kutinga fainali ya michuano hiyo.