Wawakilishi wa Afrika katika Kombe la Dunia 2026, Ivory Coast, wameaga mashindano baada ya kufungwa mabao 2-1 na Norway katika hatua ya 32 bora.
Antonio Nusa aliifungia Norway bao la kwanza dakika ya 39 kwa pasi ya nahodha Martin Ødegaard. Kipindi cha pili, Evann Guessand aliisawazishia Ivory Coast baada ya kuingia dakika ya 60 akitokea benchi.
Hata hivyo, Erling Haaland aliihakikishia Norway ushindi kwa kufunga bao la pili dakika ya 86 akimalizia pasi ya Patrick Berg.
Kwa ushindi huo, Norway imefuzu hatua ya 16 bora na sasa itakutana na Brazil, iliyoiangusha Japan kwa mabao 2-1.
