Timu ya Taifa ya Mexico imefuzu hatua ya mtoano ya michuano ya Kombe la Dunia 2026 baada ya kukusanya pointi 6 kutokana na ushindi katika michezo yake miwili ya awali, huku ikiwa imebakiza mechi moja ya mwisho ya Kundi A. Mexico ilithibitisha kufuzu baada ya kuifunga Korea Kusini mabao 1-0.
Katika msimamo wa Kundi A, Mexico inaongoza kwa pointi 6, ikifuatiwa na Korea Kusini yenye pointi 3, huku Czechia na Afrika Kusini zikiwa na pointi 1 kila moja.
Katika michezo ya mwisho ya Kundi A itakayochezwa Juni 24, Korea Kusini itavaana na Afrika Kusini, huku Mexico ikimenyana na Czechia.
