Happy Lazaro,Arusha .
Arusha .KIONGOZI wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2026, Wazo Michael Mwang’onda amezindua mradi wa ujenzi wa tenki la maji Kimondorosi lenye ujazo wa Lita elfu 50 katika Kata ya Olasiti mradi uliotelekelezwa na Mamalaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jiji la Arusha – (AUWSA ).
Akisoma taarifa ya mradi huo, Mkurugenzi Rasilimali watu, Kazimili Reuben Kanyanza amesema kuwa, mradi huo umetekelezwa na mafundi wa Mamlaka hiyo ya maji AUWSA kwa gharama ya shilingi milioni 93 huku shilingi milioni 2.5 ikiwa ni michango ya wananchi na shilingi Milioni 93.3 zikiwa ni fedha kutoka Serikali kuu.
Aidha Mwang’onda ameishukuru Serikali kwa kutekeleza miradi ya maji nchini, na kutimiza ahadi ya Mhe Rais ya Kumtua mama ndo kwa kuhakikisha huduma za maji zinawafikia wananchi kwenye maeneo yao.
Mwang’onda amefafanua kuwa,Serikali ya awamu ya sita inatekeleza ahadi zake kwa vitendo kwa kutoa fedha nyingi za kutekeleza miradi ya maji nchini huku Mhe.Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan akidhamiria kumtua mama ndoo kichwani kama ilivyo kwa wakazi wa Kimondorosi.
“Tunamshukuru Mhe Rais kwa kuhakikisha wananchi wanapata maji karibu na maeneo yao, leo Kina mama wa Kimondorosi wanakiri kuondokana na adha ya kwenda kutafuta maji mbali kitendo ambacho walikuwa wakikutana na adha kubwa huko ila kwa sasa wameweza kabisa kuondokana na changamoto hiyo.”amesema .
Awali Katika halmashauri ya wilaya ya Arusha Mwenge wa Uhuru umekimbizwa umbali wa Km 89.2 na kutembelea jumla ya miradi 7 yenye thamani ya shilingi Bilioni 3.9.
“Kauli Mbiu ya Mwenge wa Uhuru 2026 ‘Tanzania ni Yetu Sote, Tushikamane kwa Pamoja Kuijenga'”.

