Timu ya Taifa ya Afrika Kusini imefanikiwa kutoka sare ya mabao 1-1 dhidi ya Czechia katika mchezo wa hatua ya makundi ya Kombe la Dunia 2026 uliochezwa leo, Juni 18, nchini Mexico.
Afrika Kusini, ambao wapo Kundi A, wamefikisha alama moja baada ya matokeo hayo na kwa sasa wanashika nafasi ya mwisho kwenye kundi hilo.

Huu ulikuwa mchezo wao wa pili kwenye mashindano hayo, baada ya kupoteza mchezo wa kwanza kwa mabao 2-0 dhidi ya Mexico.
