Na. Fullshangwe Blog, Updates Michezo
Timu ya Taifa ya Ufaransa imeanza vyema kampeni yake ya Kombe la Dunia 2026 baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Senegal katika mchezo wa Kundi I uliochezwa Juni 16, 2026 nchini Marekani.
Baada ya kipindi cha kwanza kumalizika kwa sare ya bila kufungana, Ufaransa iliongeza kasi kipindi cha pili na kufungua ukurasa wa mabao kupitia nahodha wake, Kylian Mbappé, aliyefunga dakika ya 66. Mshambuliaji huyo alirejea tena wavuni dakika za nyongeza na kufunga bao lake la pili huku Bradley Barcola akiongeza bao lingine, na kuifanya Ufaransa kuondoka na pointi tatu muhimu. 
