Na Happy Lazaro,Arusha .

Kampuni ya Zara Adventures  Tours Tanzania imeendelea kung’ara katika maonesho ya utalii ya Karibu -Kilifair yanayoendelea jijini Arusha huku ikipongeza waandaji wa maonesho hayo kwani yamekuwa chachu katika kukuza utalii wa Tanzania .
Aidha kampuni hiyo pia   imeandaa zawadi nono kwa washiriki wa Kilimanjaro Summit Challenge na wageni wanaotembelea banda lao katika KiliFair 2026, ikiwa ni njia ya kuthamini ushiriki wao na kuendelea kuhamasisha utalii nchini.
Akizungumza katika maonesho hayo  Miongoni mwa watumishi wa Zara Adventures Tours Tanzania, Nacy Mbotea amesema kampuni hiyo imefurahishwa na mafanikio ya KiliFair 2026 pamoja na mchango wake katika kukuza sekta ya utalii nchini.

Amesema  kuwa kampuni hiyo  ni miongoni mwa wadhamini wa Kilimanjaro Summit Challenge, programu maalum inayowapa washiriki wa KiliFair fursa ya kushiriki safari ya kupanda Mlima Kilimanjaro na kujionea vivutio vya kipekee vinavyopatikana nchini Tanzania.

Nacy amesema kuwa ,ushiriki wa kampuni hiyo katika Kilimanjaro Summit Challenge umechangia kwa kiasi kikubwa kuitangaza Tanzania kimataifa kupitia utalii wa mlima, michezo ya nje na kuimarisha ushirikiano kati ya wadau wa sekta ya utalii duniani.

Aidha kampuni hiyo   imeendelea kung’ara katika Maonyesho ya Kimataifa ya Utalii ya KiliFair 2026 yanayofanyika jijini Arusha, huku ikionyesha uwezo wake mkubwa wa kuwahudumia wageni mbalimbali kutoka ndani na nje ya Tanzania waliofika kushiriki maonyesho hayo.

Nacy amesema kuwa Zara Adventures Tours Tanzania, kama mmoja wa wadau na washiriki wa maonyesho hayo, imeridhishwa na maandalizi na uendeshaji wa KiliFair 2026 ambao umewezesha kuwakutanisha wadau wa utalii kutoka Tanzania na mataifa mbalimbali duniani.

“Tumefurahi kuona wageni na washiriki kutoka mataifa mbalimbali wakifika nchini Tanzania kushiriki maonyesho haya sambamba na kupata fursa ya kutembelea banda letu na kuweza kujua huduma tunazotoa kwa ajili ya ushirikiano zaidi.”amesema .

Aidha, ametoa pongezi kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa juhudi kubwa zinazoendelea kufanyika katika kuimarisha na kutangaza utalii wa Tanzania katika soko la kimataifa.

“Tunaendelea kushuhudia matokeo chanya ya juhudi hizi. Idadi ya watalii wanaofika nchini inaongezeka, na matukio makubwa kama KiliFair yanafungua fursa zaidi za biashara, uwekezaji na ushirikiano katika sekta ya utalii,” ameongeza .

Aidha Nacy   amewashukuru waandaaji wa KiliFair 2026, washirika, wadhamini na wadau wote waliofanikisha maonyesho hayo pamoja na Kilimanjaro Summit Challenge, akieleza kuwa ushirikiano huo umechangia kuimarisha taswira ya Tanzania kama moja ya nchi bora za utalii duniani.

Amesema kampuni hiyo  itaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali katika kuendeleza utalii endelevu na kuitangaza Tanzania kama kitovu cha vivutio vya utalii barani Afrika na duniani kwa ujumla.