Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano Wa Tanzania Mhe. Balozi Dkt Emmanuel Nchimbi ameitaka Wizara ya Maji kutekeleza miradi ya maji kwa kulinda ardhi oevu nchini.
Ametoa agizo hilo katika Siku ya Mazingira iliyofanyika katika ukumbi wa Jakaya Kikwete Jijini Dodoma.
Mhe. Dkt. Nchimbi amemwakilisha Rais katika maadhimisho hayo.
Amesema hadi kufika mwaka 2050 Tanzania inakadiriwa kuwa na idadi ya watu zaidi ya milioni 100 hivyo, utunzwaji wa ardhi oevu utasaidia kuendeleza vyanzo vya maji na kupunguza upungufu wa maji.
Pia, ametoa agizo pia kwa Wakala wa Misitu Nchini (TFS) kuhakikisha miti ya kutosha inaoteshwa katika maeneo mbalimbali kwa lengo la kutunza mazingira na vyanzo vya maji.
Dira ya mwaka 2050 imejumuisha maendeleo ya mazingira na uhifadhi wa ardhi oevu Nchini.
Katika maagizo mengine makamu wa Rais ameziagiza Mamlaka za Serikali za Mitaa nchini kuanzisha bustani za kijani na kuzitunza kikamilifu.
Maadhimisho ya Siku ya Mazingira yamehusisha uzinduaji wa program endelevu ya Usimamizi wa Mazingira kuelekea Dira ya mwaka (2050) ambayo itatekelezwa kuanzia mwaka 2026 mpaka mwaka 2030.

