Mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara NBC Premier League umemalizika kwa vigogo hao wawili kutoshana nguvu ndani ya dakika 90, kila upande ukishindwa kutikisa nyavu.
Mchezo huo umepigwa Leo Machi 18, 2026 ambapo Ubao wa Uwanja wa Sheikh Amri Abeid Stadium Mkoani Arusha ulisoma: TRA United 0-0 Yanga SC na kufanya timu hizo mbili kugawana pointi moja moja baada ya pambano kali lisilozaa mabao.
Kiungo mkabaji wa TRA United, Mzamiru Yassin, alionyeshwa kadi mbili za njano zilizopelekea kadi nyekundu dakika ya 85, akiiacha timu yake pungufu uwanjani katika dakika za mwisho.
Sare hiyo inaifanya Yanga SC kuendeleza rekodi yao bora ya kutofungwa, wakifikisha mechi 15 mfululizo bila kupoteza ndani ya ligi msimu wa 2025/26. Wanajikusanyia pointi 37 na kuendelea kuongoza msimamo wa ligi.
Kwa upande wa TRA United, wamefikisha pointi 20 baada ya kucheza mechi 15, wakibaki nafasi ya 10 kwenye msimamo wa ligi.



