Simba SC imeibuka na ushindi wa mabao 2–1 dhidi ya Singida Black Stars katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC uliochezwa Uwanja wa Airtel Machi 11, 2026 Mkoani Singida.
Simba SC walianza vyema katika mchezo huo kwa kupata bao la mapema dakika ya 7 lililofungwa na Anicet Oura, akiiandikia timu yake bao la kuongoza.
Singida Black Stars walijitahidi na
Dakika ya 38 kupitia kwa Mossi na kuwafanya kwenda mapumziko wakiwa na sare ya bao moja kwa moja.
Kipindi cha pili Simba SC waliongeza juhudi za kusaka mabao, na hatimaye juhudi zao zilizaa matunda dakika ya 85 baada ya Ellie Mpanzu kufunga bao la pili na kufanya matokeo kuwa 2–1 hadi mwisho wa mchezo.
Kwa mujibu wa takwimu za mchezo huo, umiliki wa mpira ulikuwa sawa kwa pande zote mbili kwa asilimia 50 kwa 50. Singida Black Stars walipata kona 5 huku Simba SC wakipata kona 6.
Kwa upande wa mashuti yaliyolenga lango, Singida Black Stars walipiga mashuti 4 dhidi ya 6 ya Simba SC. Mashuti ambayo hayakulenga lango yalikuwa 3 kwa Singida Black Stars na 2 kwa Simba SC.
Ushindi huo unaifanya Simba SC kuondoka na alama tatu muhimu katika mbio za ligi.




