Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa anayeshughulikia Afya Prof.Tumaini Nagu amekutana na ugeni kutoka Shirika la Nutrition International.
Prof. Nagu amekutana nao leo tarehe 4 Februari, 2026 Dodoma kwa lengo la kujadili kuendelea kushirikiana na Serikali ili kuimarisha huduma za lishe nchini.
Prof. amesema, Serikali inalishukuru Shirika hilo kwa kuendelea kuunga mkono juhudi za Serikali katika kukabiliana na matatizo ya lishe nchini na amesema Serikali inatambua mchango wa Shirika hilo katika kuimarisha huduma za lishe.
Aidha amesema, Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI itaendelea kushirikiana na Shirika la Nutrition International katika kuimarisha huduma za lishe kwenye ngazi zote za Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa.
Naye Mwakilishi wa Shirika la Nutrition International Bw. Sergio Cooper amesema, Shirika hilo lipo tayari kuendelea kuunga mkono na kuchangia juhudi za Serikali za kuimarisha huduma za lishe hususani katika ngazi ya Kitaifa na ngazi ya Jamii.




