Na Hellen Mereko,
Mwanza
Baada ya kupokelewa mapema leo mkoani Mwanza, Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bara, Ndugu John Mongella, kwa niaba ya Katibu Mkuu CCM Mhe. Balozi. Asha-Rose Migiro, amekutana na kuzungumza na Viongozi wa Mashina ya CCM (Mabalozi) kutoka Wilaya za Nyamagana na Ilemela.
Katika kikao hicho, Mongella amesisitiza umuhimu wa kuimarisha uhai wa Chama kuanzia ngazi ya Shina, akiwataka Viongozi hao kuendelea kuwa nguzo ya Mshikamano, Umoja na Uhamasishaji wa Wanachama kwa kuzingatia Katiba, Maadili na Misingi ya CCM.
Ziara ya Mongella mkoani Mwanza inaendelea, ambapo anatarajiwa kuwa Mgeni Rasmi katika sherehe za maadhimisho ya miaka 49 tangu kuzaliwa kwa Chama Cha Mapinduzi. Kilele cha maadhimisho hayo kwa Mkoa wa Mwanza kitafanyika katika Jimbo la Sumve, Wilaya ya Kwimba kupitia Mkutano Mkuu wa Hadhara utakaofanyika tarehe 05 Februari, 2026.
Maadhimisho ya miaka 49 ya CCM yanaongozwa na kauli mbiu isemayo: “TUMECHAGUA UMOJA NA AMANI KWA MAENDELEO YA TAIFA LETU.”




