
Makamu Mkuu wa Chuo cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili ( MUHAS) Prof. Appolinary Kamuhabwa, akizungumza na waandishi wa habari leo Oktoba 27, 2025 jijini Dar es Salaam wakati wa ziara ya kukagua utekelezaji wa mradi wa elimu ya juu kwa Mageuzi ya kiuchumi (HEET) unaoendelea katika Kampasi ya Mloganzila.

Mratibu wa Mradi wa elimu ya juu kwa Mageuzi ya kiuchumi (HEET) MUHAS, Profesa Erasto Mbugi akizungumza na waandishi wa habari wakati wa ziara ya kukagua utekelezaji wa miradi unaoendelea katika Kampasi ya Mloganzila.


Makamu Mkuu wa Chuo MUHAS, Profesa Appolinary Kamuhabwa akiwa na Mratibu wa Mradi wa HEET, Profesa Erasto Mbugi, Wafanyakazi wa MUHAS pamoja baadhi ya wananchi wa Wilaya ya Ubungo wakikagua utekelezaji wa mradi wa elimu ya juu kwa Mageuzi ya kiuchumi (HEET) unaoendelea katika Kampasi ya Mloganzila.

Muonekano wa majengo ya Ndaki ya Tiba, Kampasi ya Mlonganzila yanayotekelezwa mradi wa HEET
…………
Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) kupitia Mradi wa Elimu ya Juu kwa Mageuzi ya Kiuchumi (HEET) unaotekeleza ujenzi wa Ndaki ya Tiba, Kampasi za Mloganzila na Kigoma, umeleta tija kwa Taifa kwa kufanya maboresho ya mitaala na kuanzisha mitaala mipya jambo ambalo limepunguza gharama za matibabu sekta ya ambazo wananchi wangekuwa wanaingia kwenda kufata huduma nje ya Nchi.
Akizungumza na waandishi wa habari leo, Oktoba 27, 2025, jijini Dar es Salaam wakati wa ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa Ndaki ya Tiba, Kampasi ya Mlogazila, Makamu Mkuu wa Chuo MUHAS, Profesa Appolinary Kamuhabwa, amesema kuwa mradi wa HEET kwa upande wa Mlonganzila ndaki ya Tiba umehusisha ujenzi wa kambi za mihadhara yenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 1, 400, Jengo la Utawala lenye ofisi za watumiaji 450, Maabara lenye Maabara 21 za kufundishia.
Profesa Kamuhabwa, amesema kuwa kukamilika kwa mradi huo kutaiwezesha MUHAS kuongeza idadi ya wanafunzi wa fani za afya kutoka 350 hadi 1,000 kwa mwaka.
Profesa Kamuhabwa amebainisha kuwa kupitia mradi wa HEET, jumla ya mitaala 83 imefanyiwa maboresho na mitaala mipya 23 imeanzishwa ili kujibu changamoto za afya nchini na kupanua wigo wa taaluma zitolewazo na MUHAS.
“Kupitia mradi wa HEET, wahadhiri 33 wamepelekwa katika mafunzo ya muda mrefu ngazi za uzamili na uzamivu, ndani na nje ya nchi, kwa lengo la kuimarisha uwezo wa kufanya tafiti za kisayansi,” amesema Profesa Kamuhabwa.
Amesema mradi huo utachangia kukuza utalii tiba kupitia vituo vya moyo, figo na saratani ya shingo ya kizazi, sambamba na kupunguza rufaa za wagonjwa nje ya nchi na hivyo kuongeza mapato ya Taifa.
Mratibu wa Mradi wa HEET MUHAS, Profesa Erasto Mbugi, amesema kukamilika kwa majengo hayo kutarahisisha upatikanaji wa mazingira bora ya kujifunzia kwa wanafunzi wa sekta ya afya, jambo litakalopunguza gharama na kuongeza ubora wa mafunzo.
Kwa upande wao Wananchi wa maeneo jirani na mradi huo, wamesema kuwa ujenzi wa mradi umefungua fursa nyingi za ajira na kuongeza kipato, huku wakitoa shukrani kwa Serikali kwa kuleta maendeleo makubwa kwa vijana na jamii kwa ujumla.
Katika ujenzi wa Ndaki ya Tiba wamejenga jengo la anatomia lenye uwezo wa watumiaji 300 kwa wakati mmoja, Bweni ya wanafunzi lenye uwezo wa kuchukua watumiaji 320, Bwalo la chakula uwezo wa kuchukua watumiaji 550 kwa wakati mmoja, Mktaba na TEHEMA lenye uwezo wa kuchukua watumiaji 550 Kwa wakati mmoja.
Pia ujenzi wa miundombinu ya barabarani pamoja na uwanja wa mpira wa miguu.
Kwa upande wa Kampasi ya Kigoma imeusisha ujenzi wa jengo la utawala na taaluma lenye uwezo wa ofisi za watumiaji 120, ukumbi wa mihadhara wenye uwezo wa watumiaji 300, Maktaba ya watumiaji 60 na TEHAMA.
Jengo la Maabara, lenye Maabara sita za kufundishia zenye uwezo wa kuchukua watumiaji 60 kila moja, jengo la anatomia lenye uwezo wa kuchukua watumiaji 300 Kwa wakati mmoja, Bweni ya wanafunzi lenye uwezo wa kuchukua watumiaji 110.
Pia ujenzi wa bwalo la chakula lenye uwezo wa watumiaji 150 kwa wakati mmoja, ujenzi wa miundombinu ya barabarani pamoja na ujenzi wa Uwanja wa Mpira wa Miguu.



