Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Dkt. Asha Rose Migiro akiwasili kwenye mkutano wa kampeni wa Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kwa tiketi ya CCM Dkt. Samia Suluhu Hassan unaofanyika kwenye uwanja wa Kecha Kinyerezi wilayani Ilala mkoa wa Dar es salaam.
Dkt. Samia anatarajiwa kunadi ilani ya uchaguzi ya CCM ya 2025/ 2030 na kuelezea utekelezaji wa ilani iliyopita sambamba na kuomba ridhaa ya Watanzania kumchagua kwa kura nyingi za ndiyo katika uchaguzi mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani ifikapo Oktoba 29, 2025.