Mgombea wa nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Rais Dkt. 𝗦𝗮𝗺𝗶𝗮 𝗦𝘂𝗹𝘂𝗵𝘂 𝗛𝗮𝘀𝘀𝗮𝗻 amepokelewa na maelfu ya wananchi wa Muleba mkoani Kagera walioujaza uwanja wa Zimbile wakiwa na shauku na hamasa kubwa ya kumahakikishia ushindi wa kishindo ifikapo Oktoba 29 katika uchaguzi mkuu.
Sehemu ya Wananchi wa Muleba mkoani Kagera waliohudhuria mkutano wa hadhara wa Kampeni wa Mgombea wa nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa Ndugu Dkt. Samia Suluhu Hassan, tarehe 15 Oktoba, 2025.
Shamra shamra za mapokezi ya Mgombea wa nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa Ndugu Dkt. Samia Suluhu Hassan mara baada ya kuwasili Muleba mkoani Kagera tarehe 15 Oktoba, 2025.