MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akihutubia maelfu ya wananchi wa Wilaya ya Meatu katika mkutano mkubwa wa hadhara, uliofanyika kiwanja cha kituo cha mabasi mji wa Mwanhuzi, leo Jumanne tarehe 17 Juni 2025, ukiwa ni muendelezo wa ziara yake ya kikazi ya siku tano mkoani Simiyu.
Kabla ya kuzungumza na wananchi hao, Mhe. Dkt. Samia alifungua Kiwanda cha Kuchakata Pamba cha Biosustain Tanzania Limited, kilichoko wilayani humo.