Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko ameshiriki katika hafla ya kupokea gawio na michango kutoka kwa Taasisi na Mashirika ya Umma na Kampuni ambazo Serikali ina hisa zake
Hafla hiyo imefanyika leo Juni 10, 2025 Ikulu jijini Dar es salaam na kupokelewa na mgeni rasmi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.