Waziri wa habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe. Tabia Maulid Mwita akifungua Kongamano la Wadau wa Utangazaji Zanzibar katika Ukumbi wa sheikh Idrisa Abdulwakil.Kikwajuni,Wilaya ya Mjini.
Mwenyekiti wa Tume ya Utangazaji Sleiman Ame Khamis akitoa maelezo kwa wadau wa Utangazaji Zanzibar katika Ukumbi wa sheikh Idrisa Abdulwakil.Kikwajuni,Wilaya ya Mjini.
Meneja wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania ( TCRA ) Kanda ya Zanzibar Bi Esuvatie Masinga akiielezea mashirikiano yaliopo na Tume ya Utangazaji Zanzibar katika Ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdulwakil.Kikwajuni,Wilaya ya Mjini.

Baadhi ya Wadau wa Utangazaji Zanzibar wakimsikiliza. Waziri wa habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe. Tabia Maulid Mwita (hayupo pichani ) katika Ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdulwakil.Kikwajuni,Wilaya ya Mjini.
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe. Tabia Maulid Mwita akimkabidhi zawadi Katibu Mtendaji wa Tume ya Utangazaji Zanzibar Hiji Dadi Shajak aliyotunukiwa na wafanyakazi wa Tume ya Utangazaji katika Ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdulwakil.Kikwajuni,Wilaya ya Mjini.
……………
Waziri wa habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe. Tabia Maulid Mwita
amevitaka vyombo vya habari kuripoti Sera na Ilani ya vyama vya siasa ili Wananchi waweze kupata elimu ya kutosha.
Ameyasema hayo, huko katika Ukumbi wa Sheikh Idrissa Abdulwakil Kikwajuni wakati wa ufunguzi wa Kongamano la Vituo vya Utangazaji Zanzibar.
Amesema utoaji wa elimu hiyo, itawawezesha Wananchi kuchaguwa Viongozi wanaofaa.
Aidha amesema baadhi ya Waandishi wanatumiwa na vyama vya siasa katika kueneza propaganda za chuki na uhasama kwa Wananchi.
Amefahamisha kuwa, Tume ya Utangazaji Zanzibar, inadhamana ya kutoa leseni za Utangazaji, kudhibiti shughuli za utangazaji, maadili hivyo amewataka Waandishi kulinda Sera, Usalama, Mila na Utamaduni wa Zanzibar.
Hata hivyo ametoa Witoa Kwa vyombo vya Utangazaji Zanzibar kuandaa maudhui yanayowahamasisha Wananchi kushiriki katika Uchaguzi kwa Amani na Utulivu.
Aidha amezitaka Taasisi husika na kuandaa mkakati maalum, utakaosaidia kujadili changamoto za kisekta ili kuweza kuenda sambamba na wakati uliopo wa Sayansi na Teknolojia.
Nae Katibu Mtendaji Tume ya Utangazaji Zanzibar Hiji Dadi Shajak, amesema lengo la Kongamano hilo ni kuimarisha mashirikiano na wadau wa Vituo vya Utangazaji ili kuleta mustakbaki mwema kwa tasnia ya habari
Amesema iwapo Vituo hivyo vitafuata maadili ya Utangazaji ipasavyo, vitasaidia kulinda Amani ya nchi kabla, wakati na baada ya Uchaguzi .
Mwenyekiti wa Tume ya Utangazaji Sleiman Ame Khamis amefahamisha kwamba mashirikiano na mshikamano na wadau Mbali mbali utasaidia kuleta maendeleo katika sekta ya Utangazaji.
Nae Meneja wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania ( TCRA ) Ofisi ya Zanzibar Bi Esuvatie Masinga amesema wamekuwa wakifanya kazi nyingi pamoja na Tume ya Utangazaji Zanzibar ikiwemo kutoa elimu kwa jamii.
Hivyo ameishukuru Tume ya Utangazaji Zanzibar na kuahidi kushirikiana ili waweze kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi
Tunzo mbalimbali zimetolewa ikiwemo, vinara waliotoa huduma bora kwa jamii, vituo vilivyolipa kodi vizuri ambapo Mhe. Tabia ameahidi kutoa fedha ili kuongeza Ari na Motisha katika vituo vya Utangazaji.
Kauli mbiu ya Kongamano Hilo ni “Zingatia maadili ya Utangazaji tulinde Amani Utulivu wa nchi yetu “