SALAMU ZA PONGEZI
Nimepokea kwa furaha kubwa taarifa za kuteuliwa kwa Dkt. Deo Osmund Mwapinga kuwa Katibu Mkuu wa Jukwaa la Mabunge ya Mkutano wa Kimataifa wa Ukanda wa Maziwa Makuu (FP-ICGLR). Dkt. Mwapinga ameteuliwa na Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa 15 wa Jukwaa hilo uliofanyika tarehe 25 Aprili, 2025 Luanda, Angola.
Nachukua fursa hii kumpongeza kwa dhati Dkt. Mwapinga kwa kuaminiwa na Wajumbe wa Jumuiya ya Mabunge ya Nchi Wanachama wa Jukwaa hilo kushika wadhifa huu adhimu.
Uteuzi wake ni kielelezo cha imani na matumaini waliyonayo Wajumbe wa Mabunge Wanachama wa Jukwaa la Maziwa Makuu juu ya uwezo, uadilifu na umahiri wake pamoja na dhamira ya Tanzania katika kuimarisha ushirikiano wa kikanda.
Namtakia kila la heri na kumuahidi ushirikiano wangu katika utekelezaji wa majukumu yake.
Baraka I. Leonard
KATIBU WA BUNGE