Mwenyekiti wa chama cha demokrasia na maendeleo Chadema akizungumza na wananchi wa mkoa wa Rukwa
Baadhi ya wananchi walioshiriki katika uzinduzi wa kampeni ya no reform no election
………………..
Na Neema Mtuka sumbawanga
Rukwa : Mwenyekiti wa chama cha demokrasia na maendeleo Chadema Tundu Antipas Lissu ametaka uchaguzi mkuu wa mwaka huu kuwa wa uwazi na huru.
Akizungumza leo March 26 ,2025 katika uwanja wa shule ya msiñgi Ndua amesema kuwa bila mabadiliko hakuna uchaguzi kauli hiyo itawafikisha mbali na yupo tayari kuongoza hayo mapambano.
Amesema mabadiliko wanayoyataka sio mapya bali lengo lao ni kuendelea kulinda amani iliyopo na kutunza tunu za taifa.
Mbunge wa jimbo la Nkasi kaskazini Aidah Kenani amesema wananchi wanahitaji mabadiliko ya haraka ili kuondokana na changamoto mbalimbali ikiwemo ajira kwa vijana.
Mwenyekiti wa Kanda ya Nyasa Joseph Mbilinyi amesema wapo kwenye oparesheni katika kila Kanda kuzindua kampeni ya (no reform no election )hakuna mabadiliko hakuna uchaguzi.
Amesema kanda ya Nyasa ndio ngome katika kanda zote na wameamua kufanya mabadiliko ya kweli.
Amewataka wanachama wa chama hicho kukubali kufanya mabadiliko yatakayoleta tija kwa watanzania wote.
Akiwa mjini sumbawanga Tundu Lissu amekutana na kuzungumza na wananchi , wanachama na viongozi mbalimbali wa dini.
Nao baadhi ya wanachama wa chama cha demokrasia na maendeleo Chadema Ashura Miraji amesema kwa umoja wao wanaweza kuleta mabadiliko makubwa kiasi cha kuushangaza ulimwengu.
“Chadema ni chama chenye nguvu kwa umoja wetu tunaweza kubadili taswira iliyojengeka kuwa hatuwezi.”amesema Miraji.
Mwenyekiti wa Baraza la vijana wa Chadema mkoa wa Rukwa Benjamin Mizengo amesema ujio wa kiongozi huyo wa kitaifa utaleta chachu katika kuimarisha chama chao kwa kuwa wana imani nae.
“Mabadiliko yanaanza na sisi tukikubaliana kwa pamoja kampeni hii itafanikiwa kwa kiasi kikubwa na kupata matokeo yenye tija kwa Jamii.