Mkoa wa Mjini Magharibi.
Mjumbe wa Halmashauri kuu ya Chama Cha Mapinduzi (NEC) Mhe. Tabia Maulid Mwita amewataka Watendaji wa (UWT) kushirikiana ili kufanikisha zoezi la Uandikishaji wa Daftari la kudumu la Wapiga kura, linalotarajiwa kuanza tarehe 15 mwezi huu, katika Mkoa wa Mjini Kichama.
Mhe. Tabia ambae pia ni Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo ameyasema hayo huko Amani katika Ofisi ya CCM Mkoa wa Mjini kichama mara baada ya kukabidhi fedha Taslim Sh. Milioni 3 kwa Kamati tekelezaji UWT Mkoa, Wilaya Mjini na Amani kichama.
Amesema Watendaji hao, wanafanya kazi nzuri ya kuhamasisha Vijana hivyo ameamua kutoa fedha hizo ili kuunga mkono juhudi wwanazozifanya.
Mbali na hayo Mhe. Tabia amesema anatarajia kusaidia Majimbo yote 9 ya Mkoa huo kwa ajili ya Daftari li kusaidia harakati za kuendesha zoezi hilo.
‘‘Najuwa Chama Cha Mapinduzi na Jumuiya zake kimejipanga vizuri kwa Daftari ila na mimi nataka niwe sehemu ya kusaidia Jumuiya yetu hii’’ alisema Waziri Tabaia.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Mjini kichama Ghanima Sheha Mbwara na Katibu wa UWT Mkoani humo, Mary Pius Miwa wamesema wamejipanga kuhakikisha Vijana wote wenye sifa wanaandikishwa ili Mkoa wa Mjini uweze kushika nambari moja.
Akitoa shukrani kwa niaba ya Watendaji wenzake, Mjumbe wa Baraza kuu UWT Mkoa wa Mjini kichama Salma Ibada amesema msaada huo, umekuja wakati muafaka na kuahidi kuutumia kama ulivyokusudiwa.
Hata hivyo amesema msaada huo umeongeza ari na motisha katika utendaji wa kazi na kuahidi kushirikiana kuwa bega kwa bega ili kuhakikisha zoezi hilo kwa maslah ya UWT na Chama kwa Ujumla.
Zoezi la Uandikishaji wa Daftari la kudumu la wapiga kura kwa upande wa Mkoa wa Mjini kichama, ilinarajiwa kuanza tarehe 15 mwezi huu.

