Mabingwa Watetezi wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara Yanga Sc wameibuka na ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Mashujaa Fc katika mchezo wa ligi kuu uliopigwa leo Disemba 19, 2024 katika Uwanja wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni KMC Complex uliopo Mwenge Jijini Dar es Salaam.
Mabao ya Yanga SC yamefungwa na Mshambuliaji wa Kimataifa wa Zimbambe, Prince Dube Mpumelelo aliyefunga mabao yote matatu dakika ya saba, 21, 54, huku Mabao ya Mshujaa yakifungwa na David Ulomi dakika ya 45 na Idrisa Stambuli dakika ya 62.
Kwa ushindi huo Yanga SC imefikisha pointi 30 na kurejea nafasi ya tatu, ikizidiwa pointi moja na wastani wao Simba SC baada ya wote kucheza michezo 12.
Kwa upande wao Mashujaa baada ya kupoteza mchezo wa leo wanabaki na pointi 15 wakiwa nafasi ya saba katika msimamo wa ligi kuu.