Afisa Ubalozi wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Nchini China Dk,Miraji Ukuti Ussi akizungumza katika hafla ya Uzinduzi wa Mashindano ya Mbio za Marathon zitakazofadhiliwa na Kampuni ya Touch Road China ambazo zinatarajiwa kufanyika 27Disemba 2024 zenye kauli mbiu “KUFIKIRIA UPYA WIGO WA UTALII”hafla iliofanyika katika ukumbi wa Idriss Abdul Wakil Kikwajuni Zanzibar.
Mwenyekiti wa Kampuni ya Touch Road China Dk He Liehui akitoa maelezo kuhusiana na Mashindano ya Mbio za Marathon zitakazofadhiliwa na Kampuni hio zinazotarajiwa kufanyika 27Disemba 2024 zenye kauli mbiu “KUFIKIRIA UPYA WIGO WA UTALII”hafla iliofanyika katika ukumbi wa Idriss Abdul Wakil Kikwajuni Zanzibar.
Katibu Mkuu Wizara ya Utalii na Mambo ya Kale Dk Aboud Suleiman Jumbe akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusiana na Mashindano ya Mbio za Marathon zitakazofadhiliwa na Kampuni hio zinazotarajiwa kufanyika 27Disemba 2024 zenye kauli mbiu “KUFIKIRIA UPYA WIGO WA UTALII”hafla iliofanyika katika ukumbi wa Idriss Abdul Wakil Kikwajuni Zanzibar.
Katibu Mkuu Wizara ya Utalii na Mambo ya Kale Dk Aboud Suleiman Jumbe akikabidhiwa Fulana na Mwenyekiti wa Kampuni ya Touch Road China Dk He Liehui ambazo zitatumika katika Mashindano ya Mbio za Marathon zinazotarajiwa kufanyika 27Disemba 2024 zenye kauli mbiu “KUFIKIRIA UPYA WIGO WA UTALII”hafla iliofanyika katika ukumbi wa Idriss Abdul Wakil Kikwajuni Zanzibar.
PICHA NO-2600-Katibu Mkuu Wizara ya Utalii na Mambo ya Kale Dk Aboud Suleiman Jumbe akiwa katika Picha ya pamoja na Viongozi mbalimbali katika hafla ya Uzinduzi wa Mashindano ya Mbio za Marathon zitakazofadhiliwa na Kampuni ya Touch Road China ambazo zinatarajiwa kufanyika 27Disemba 2024 zenye kauli mbiu “KUFIKIRIA UPYA WIGO WA UTALII”hafla iliofanyika katika ukumbi wa Idriss Abdul Wakil Kikwajuni Zanzibar. (PICHA NA YUSSUF SIMAI,MAELEZO ZANZIBAR.22/11/2024)
………….
Na Rahma Khamis Maelezo 22/11/2024
Katibu Mkuu Wizara ya Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar Dkt Abuod Sueiman Jumbe amewataka wananchi kujitoka kwa wingi kushiriki katika mchezo wa mbio za Marathon zinazotarajiwa kufanyika Novemba 27 2024.
Wito huo ameutoa katika Ukumbi wa Wizara hiyo Kikwajuni wakati akizungumza na waandishi wa Habari kuhusiana na ujio wa mbio hizo za Marathon ili kuendeleza utalii nchini.
Amesema ujio wa marathon Zanzibar unafungua ukurasa mpya wa Utalii katika kuendeleza kupitia tamasha hilo.
Aidha amefahamisha kuwa ujio huo ni kutekeleza ahadi za Dkt Mwinyi katika kuutangaza Utalii na kunyayua kasi ya Utalii ili kuongeza idadi ya watalii wanaokuja Zanzibar
Katibu huyo ameeleza kuwa lengo la mbio hizo ni kupanua wigo pamoja na kuinua Uchumi wa Zanzibar na wananchi wake .
Amesema Serikali kupitia Wizara inafanya jitihada katika kuhakikisha kuwa Utalii unatangazwa ili kuongeza idadi ya wageni nchini.
Aidha amewasisistiza wananchi kujitokeza kwa wingi katika mashindano hayo ya kilomita tano, kumi, kumi na tano na kilomita ishirini (20) ambapo washindi wa kwanza hadi wa tatu watapata zawadi za fedha taslimu
Hata hivyo amesema kuwa pia wameweka mikakati ya kuongeza bidhaa zenye kivutio kwa watalii, kwa kutoa msukumo kwa upande wa historian a mambo yakale , Michezo na utalii wa vyakula vya asili na mikutano ili kuongeza siku za kukaa nchini na ongeza pato.
Nae Mwenyekiti wa Kampuni ya Touchroad International kutoka China Dkt Hi amesema kushiriki tamasha hilo pamoja ni kuendeleza uhusiano kati yao na Zanzibar ili kuimarisha utalii.
Tamasha hilo litashirikisha wageni kutoka nchi mbalimbali ikiwemo China, Ethiopia, Kenya na wenyeji wao Tanzania ambapo watapata fursa ya kutembelea sehemu mbalimbali za kitalii na kuvitangaza katika mitandao yao.