Kumekuwepo na maswali na maoni mengi kutoka kwa Waandishi wa Habari na Wananchi wakitaka kufahamu hatua iliyofikiwa ya matukio mawwili ambayo ni tukio la Deogratius Tarimo, alilofanyiwa katika eneo la Kiluvya Novemba 11,2024 Jijini Dar es Salaam na tukio linalohusu mmiliki/wamiliki wa Jengo lililoanguka huko kariakoo Novemba 16,2024.
Upelelezi wa kesi hizi mbili upo katika hatua nzuri na hivi karibuni taarifa kamili itatolewa kwa umma.
Imetolewa na:
David A. Misime – DCP
Msemaji wa Jeshi la Polisi
Makao Makuu ya Polisi
Dodoma,Tanzania.