Timu ya Taifa ya Tanzania ya Mpira wa Miguu imefanikiwa kufuzu Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) mwakani nchini Morocco baada ya ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Guinea katika mchezo wa kundi H uliochezwa leo Novemba 19, 2024 katika uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.
Mfungaji wa bao kwa Tanzania Mshambuliaji wa Al Talaba ya Iraq Simon Msuva katika dakika ya 61 ya mchezo huo akimalizia pasi ya kiungo wa klabu ya Yanga Mudathir Yahy Abbas.
Kwa ushindi huo Taifa Stars imefikisha poini 10 baada ya kucheza mechi sita katika kundi hilo na kuungana na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) yenye pointi 12.
Ni mara ya nne katika historia ya Tanzania kufuzu AFCON baada ya mwaka 1980 nchini Nigeria, 2019 Misri, 2023 Ivory Coast na mara ya kwanza kufuzu fainali mbili mfululizo.