Afisa Elimu mwandamizi wa Makumbusho ya Taifa la Tanzania, Bi. Anna Sonelo akizungumzia umuhimu wa warsha maalum iliyoandaliwa na Kitengo cha Elimu cha Makumbusho ya Taifa kwa kushirikiana na Umoja wa Wakuu wa Shule za Sekondari kanda ya Dar es Salaam (TAHOSSA) iliyofanyika katika Kituo cha Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni jijini Dar es Salaam
…………………
Makumbusho ya Taifa la Tanzania imewataka Umoja wa Shule za Sekondari (TAHOSSA) kuwapeleka wanafunzi wao kufanya utalii katika Makumbusho hiyo ili waweze kujifunza historia na uzaledo wa nchini yao.
Hayo yamejiri leo tar 26 /9/2024 katika warsha maalum iliyoandaliwa na Kitengo cha Elimu cha Makumbusho ya Taifa kwa kushirikiana na Umoja wa Wakuu wa Shule za Sekondari kanda ya Dar es Salaam (TAHOSSA) iliyofanyika katika Kituo cha Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni jijini Dar es Salaam kwa lengo la kubadilishana uzoefu katika masuala mbali mbali yanayohusu uendeshaji wa shule na namna bora ya kufundisha na kuendeleza maadili, uzalendo na malezi ya Kitanzania kwa watoto.
Akizungumza katika warsha hiyo Afisa Elimu mwandamizi wa Makumbusho ya Taifa la Tanzania, Bi. Anna Sonelo amesema dhamira ya Taasisi hiyo ni kuhakikisha walimu na wanafunzi wanahamasika kutembelea Makumbusho na maeneo ya malikale kwa ajili ya kujifunza na kujionea urithi wa utamaduni na historia ya Tanzania.
Bi. Sonelo amezitaja huduma mbalimbali zinazotolewa kwa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari kuwa ni pamoja na kampeni ya ‘Twenzetu Makumbusho’ kwa lengo la kuhamasisha umma kwa ujumla kutembelea Makumbusho ya Taifa kwa lengo la kujifunza na kuburudika kutokana na urithi wa historia na Utamaduni uliohifadhiwa,kazi miradi kwa wafunzi wa vidato vya mitihani,kumbi kwa aijili mahafali kwa shule za msingi na sekondari.
“Pia kuna huduma ya kutembelea vivutio vya asili na historia ya jiji la Dar es Salaam (Dar es Salaam City Tour ).
Aidha Makumbusho ya Taifa la Tanzania ina program maluumu za kieliemu kwa kutembelea taasisi za elimu (Outreach programu ) kwa ajili ya kutoa elimu ya kimakumbusho kwa ujumla,
Amesema pia kuna gari ya Makumbusho inayotembea ambalo huambatana na zana za asili zilizotumika katika nyakati za zamani kama vile kusaga na kukata nyama kwa kutumia zana za mawe, ususi na ufinyazi.
Afisa elimu huyo wa Makumbusho amessisitiza kuwa mipango yao ni kuhakikisha wanafunzi wanatumia fursa za programu maalumu za kielimu, mafunzo kwa vitendo kwenye baiolojiana akiolojia, huduma za maktaba na mambo mengine yanayohusiana na hayo yanatumika kikamilifu kwa ustawi wa Taifa la Tanzania.
Kwa upande wake Afisa Elimu Mkoa wa Dar es Salaam, Bw. Gift Kyando akifungua warsha hiyo amewasisitiza walimu hao kuwafundisha wanafunzi uzalendo ikiwemo kuwapeleka Makumbusho ili wakajifunze masuala mbalimbali ya kihistoria na utamaduni wa mtanzania kwa vitendo.