Mkurugenzi  Mtendaji wa Taasisi hiyo ya Twende,John  Rexford Nzira akizungumza katika maadhimisho  hayo mkoani Arusha .
Mwenyekiti wa bodi ya TEN/MET ,Faraja Nyalandu akizungumza katika maadhimisho hayo yaliyofanyika ofisi za Taasisi  hiyo  mkoani Arusha .
Happy Lazaro,Arusha.
Arusha .TAASISI   isiyo ya kiserikali  ya Twende  inayowajengea watanzania   uwezo wa kubuni teknolojia mbalimbali zinazotumika kutatua changamoto za kila siku imetoa  mafunzo  ya ubunifu wa teknolojia kwa zaidi ya Wanafunzi  Elfu tano kutoka mikoa ya Arusha ,Kilimanjaro,na Manyara .
Aidha Taasisi hiyo imetoa  mafunzo kwa wanafunzi  hao  kuhusu   maswala ya ubunifu wa teknolojia na ujasiriamali ambapo wameweza  kubuni mashine mbalimbali  za ubunifu wakisaidiwa  na wataalamu kutoka taasisi hiyo. 
Mkurugenzi  Mtendaji wa Taasisi hiyo ya Twende,John  Rexford Nzira   ameyasema hayo leo mkoani Arusha wakati akizungumza katika maadhimisho ya miaka 10 ya  mafunzo ya  ubunifu kwa wanafunzi .
John amesema kuwa,  Taasisi hiyo ina zaidi ya  miaka 20  tangu kuanzishwa kwake ,ambapo imekuwa ikitoa mafunzo sio kwa wanafunzi tu bali kwa wanajamii wote kuhusu  maswala ya ubunifu ambapo imekuwa  na mchango mkubwa katika kutatua changamoto mbalimbali zilizopo katika jamii kwa kubuni mashine mbalimbali .
“Leo tunaadhimisha miaka 10 ya mafunzo ya ubunifu na ujasiriamali kwa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari ambapo wataalamu  wetu  hutembelea  mashuleni na kuweza kusikiliza mawazo  ya wanafunzi na kuwajengea uwezo wa ubunifu kulingana na wazo lao ambapo wamekuwa wakifanya kazi na wanafunzi zaidi ya 500 hadi 700 kwa mwaka .”amesema .
John amesema  kuwa, lengo la kuwafikia wanafunzi hao ni ili kuwawezesha kuwa wabunifu wakiwa tangu wadogo kulingana na  hali.ya maisha ya sasa hivi kwani  kupitia bunifu hizo wataweza kujiajiri wenyewe .
Kwa upande wake Mwenyekiti wa bodi ya TEN/MET ,Faraja Nyalandu amepongeza kitendo hicho kilichofanywa na taasisi hiyo kwani kinasaidia sana wanafunzi kuwa wabunifu na kuweza kuja  na miradi mbalimbali ya kutatua changamoto kwenye jamii pindi wanaohitimu masomo yao.
“Hapa tumeona namna ambavyo wanafunzi wameonyesha bunifu mbalimbali walizoweza  kubuni  kwa kuwezeshwa na taasisi hii  kwa kweli ni kitu kizuri sana katika sekta ya elimu na kinapaswa kuigwa na wengine kwani kwa dunia ya sasa hivi  tunahitaji  zaidi wabunifu katika kutatua changamoto mbalimbali katika jamii.”amesema Faraja. 
Kwa upande wa wanafunzi walionufaika na Taasisi hiyo, Julieth Marco na Haruna Miraji wamesema kuwa, taasisi hiyo imewasaidia sana wao  kuwa wabunifu kwa kubuni mashine mbalimbali ambazo zina uwezo mkubwa wa kutatua changamoto katika jamii inayowakabili. 
“Kwa mfano mimi  nimeweza  kupata elimu ya ubunifu kuhusu vitu vipya na kuweza kutengeneza mashine mbalimbali kama hii ya kuchuja maji machafu ambayo nimetengeneza na itasaidia sana kuokoa uchafuzi  wa mazingira kwenye jamii hivyo hili  ni jambo la kuigwa na taasisi mbalimbali .”amesema .