Mkuu wa Mkoa wa Arusha, CPA Amos Gabriel Makalla akizungumza na waandishi wa habari jijini Arusha leo.
……………
Happy Lazaro,Arusha .
Arusha.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kufanya ziara ya kikazi ya siku tatu Mkoani Arusha kuanzia Novemba 19 hadi 21, 2026.
Akizungumza na waandishi wa habari Ofisini kwake Jijini Arusha, Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. CPA Amos Gabriel Makalla amesema Novemba 20, Mhe. Rais Samia atafungua Mkutano wa Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Polisi utakaofanyika kwenye Chuo cha Polisi Moshi Mkoani Kilimanjaro.
Aidha CPA Makalla amebainisha kuwa Novemba 21, 2026 Mhe. Rais Samia atatunuku Kamisheni kwa Maafisa wanafunzi wa Jeshi la Ulinzi wa Wananchi wa Tanzania (JWTZ) katika Chuo cha Kijeshi Monduli Mkoani Arusha.
Katika Mkutano wake na wanahabari, Mhe. Makalla pia ametoa wito kwa wananchi wa Mkoa wa Arusha kujitokeza kwa wingi kwenye mapokezi ya Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.
