Katibu Mkuu ofisi ya Rais Utumishi ,Xavier Daud akizungumza katika mkutano huo mkoani Arusha .
…………………
Happy Lazaro,Arusha .
Arusha .Katibu Mkuu ofisi ya Rais Utumishi ,Xavier Daud amesisitiza taasisi za nchi wanachama wa (ESARBICA) kutumia teknolojia zenye mfumo wa kisasa wa utunzaji wa Nyaraka na kumbukumbu ili kuendana na teknolojia na kuongeza ufanisi katika utendaji kazi
Ameyasema hayo leo mkoani Arusha katika mkutano wa 59 wa nchi wanachama wa bodi ya baraza la wahifadhi nyaraka kusini mashariki Afrika (ESARBICA) uliozihusisha taasisi zinazohusika na utunzajia wa kumbukumbu na nyaraka.
Aidha amesisitiza kwamba kwa asili utunzaji wa nyaraka ulikuwa wa kawaida lakini kwa sasa hivi hali imebadilika na kuwa ya sayansi na teknolojia na kusababisha ufanisi kuongezeka kwa maana ya kuwa mnawasiliana haraka.
“Tunasisitiza kwamba baada ya mabadiliko ya teknolojia tutoke kwenye utunzaji wa nyaraka na kumbukumbu za serikali za makaratasi ,kama tunavyojua nyaraka na kumbukumbu ni moyo wa serikali unapotunza nyaraka zako kidigitali unakuwa na ufanisi zaidi katika utendaji kazi .”amesema.
Aidha alisisitiza taasisi za nchi wanachama na nchi ya Tanzania kuendelea kutumia mifumo hiyo ya kisasa .
Amefafanua kuwa,kutokana na mabadiliko ya kimfumo alisisitiza kuwepo kwa wataalamu wazawa na wazalendo ili wenye kuweza kumiliki mifumo yetu ili kuweza kudhibiti mifumo hiyo .
Naye Mkurugenzi ofisi ya Rais idara ya kumbukumbu na nyaraka za Taifa ,Firimin Msiangi amesema kuwa kazi ya bodi ni kubadilishana uzoefu katika kuhakikisha sekta hiyo inaboreshwa na katika kuhakikisha kumbukumbu na nyaraka za serikali katika nchi yetu inatunzwa vizuri na kutoa huduma bora kwa wananchi .
“Katika eneo hili kila nchi ina uzoefu wake ndio maana tumekutana hapa kwa ajili ya kubadilishana uzoefu “amesema Msiangi.
Amefafanua kuwa, katika mkutano huo nchi zilizoshiriki ni 14 kati ya nchi 15 wanachama na wanaendelea kuzihamasisha nchi zingine kushiriki katika mkutano huo .
Amesema kuwa,pamoja na mambo mengine mkutano huo utajadili namna wanavyoondoka kwenye matumizi ya nyaraka za karatasi kwenda kidigitali ikiwa ni hatua ya kuboresha huduma bora kwa wananchi na serikali kwa ujumla .
Kwa upande wake Rais wa ESARBICA ,Puleng Kekana kutoka nchini Afrika kusini amesema kuwa ,serikali imeanzisha usimamizi wa kumbukumbu za kidijitali na mfumo wa uhifadhi ambapo mkakati wa kuhifadhi kumbukumbu,
Amesema kuwa ,wakati wa kutekeleza upatikanaji wa kumbukumbu inapohitajika na watumiaji, kumbukumbu za Taifa daima zimeendelea kushirikiana na baadhi ya taasisi za umma, ikiwa ni pamoja na wizara, mashirika ya serikali, kuweka kumbukumbu zao kwa madhumuni ya kuhifadhi na kupatikana kwa maamuzi kwa wakati .
Kekana amefafanua kuwa,mashirika tuliyonayo yanapaswa kuhakikisha kuwa nchi wanachama zinachukua hatua madhubuti za kuandaa na kutekeleza programu za mafunzo kwa taaluma za kumbukumbu, haswa vijana, huku akiwataka wanaharakati kuhakikisha taasisi za kitaaluma katika kanda zinaboresha mitaala yao ya kumbukumbu na usimamizi wa kumbukumbu ili kuendana na ukuaji wa teknolojia ya habari na mawasiliano katika usimamizi wa kumbukumbu .