Mchumi wa Halmashauri ya Sengerema, Wilbad Bandola,leo akitoa taarifa ya mradi wa uwanja wa michezo Mnadani kwa Kamati ya Siasa ya CCM Mkoa wa Mwanza..
Mkuu wa Mkoa wa mwanza, Said Mtanda akizungumza baada ya Kamati ya Siasa ya CCM Mkoa wa Mwanza ilipokagua mradi wa uwanja wa Mnadani, leo.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mwanza, Michael Masanja ‘Smart’ akizungumza baada ya Kamati ya Siasa kutemmbelea mradi wa uwanja wa Mnadani. Picha zote na Baltazar Mashaka
…….
NA BALTAZAR MASHAKA, SENGEREMA
HALMASHAURI ya Wilaya ya Sengerema imepongezwa kwa ubunifu wa ujenzi wa uwanja wa michezo wilayani humo kuwa utachochea ukuaji wa michezo na mapato ya halmashauri hiyo.
Pongezi hizo zilitolewa leo na Mwenyekiti wa CCM Mkoawa Mwanza, Michael Masanja ‘Smart ‘ kwa niaba ya Kamati ya Siasa ya CCM Mkoa, baada ya kukagua utekelezaji wa ilani ya uchaguzi wilayani Sengerema.
“Kamati tunapongeza kwa mradi huu wa uwanja unaokidhi mahitaji ya wananchi wa Sengerema na halmashuri mtakusanya mapato sahihi kupitia michezo, pia ukikamilika mengi yatafanyika ambapo timu kubwa za Simba, Yanga na Pamba zitakuja kucheza hapa,” alisema Smart.
Alisema uwanja wa michezo Mnadani lilikuwa hitaji la wananchi muda mrefu ,hivyo serikali ya awamu ya sita na uongozi wa halmashauri kuridhia ujenzi huo kwa mapato ya ndani.
Aliwahimiza wananchi kuchapa kazi n kueleza kuwa serikali itaendelea kuleta fedha za miradi ya maendeleo wafaidi matunda ya kodi zao.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Said Mtanda, alisema serikali ni kuona mradi huo ukikamilika utasaidia kuinua michezo n mapato ya Sengerema.
“Timu ya Pamba itaweka kambi hapa pia nitamleta Diamond kuufungua rasmi, hivyo fanyeni hima mradi ukishakamilika nitaileta Pamba na Yanga hapa,Sengerema mtapata mapato hapa Mnadani,”alisema .
Awali Ofisa Uchumi na Mipango wa Halmashauri ya Sengerema, Wilbad Bandola alisema lengo la kujenga uwanja wa michezo Mnadani ni maelekezo ya ilani ya CCM, utasaidia kuibua na kukuza vipaji na kuendeleza michezo .
Mbali na kuinua sekta ya michezo pia, uwanja huo utasaidia kuongeza mapato ya halmashauri kwa viingilio vya milangoni na vibanda vya bbiashara vitakavyojengwa kuzunguka uwanja.
“Fedha za gharama za ujenzi ni sh. milioni 361.2 za mapato ya ndani, mfuko wa jimbo, ufadhili wa mbunge na wadau wa maendeleo.Awamu ya kwanza ya ujenzi utahusisha uzio na miundombinu mbalimbali , ukikamilika utakuwa n uwezo wa kubeba watazamaji 15,000 hadi 20,000 kwa wakati mmoja,”alisema Bandola.
Alisema miundombinu inayoendelea kujengwa ni uzio (ukuta), matundu 24 ya vyoo hadi sasa sh. milioni 220.5 zimepokelewa kati ya sh.milioni 361.2 na zilizokwisha kutumika kwa ujenzi huo ni sh.milioni 189