Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mwanza, Michael Masanja ‘Smart’, wa nne kutoka kushoto akizungumza jambo kabla ya kukagua mradi wa shule mpya ya Msingi Shilabela, A pili kutoka kushoto ni Katibu wa Mkoa, Omar Mtuwa.
Wajumbe wa Kamati ya Siasa ya CCM Mkoa wa Mwanza, wakitoka kukagua ujenzi wa Shule mpya ya Msingi Shilabela wakiongozwa na Mwenyekiti, Michael Masanja ‘Smart’, leo.Kushoto ni Katibu wa Mkoa Omar Mtuwa.
Mwalimu wa Taaluma Shule ya Msingi Shilabela, Modester Aloyce akitoa taarifa ya mradi wa ujenzi wa shule hiyo, leo kwa Kamati ya Siasa ya CCM Mkoa wa Mwanza.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mwanza, akizungumza na wajumbe wa Kamati ya Siasa ya Mkoa wakiwemo watumishi wa Halmashauri ya Misungwi (hawapo pichani), leo.
Mkuu wa Wilaya ya Misungwi,Johari Samizi akizungumza wakati wa majumuisho ya ziara ya Kamati ya Siasa ya Mkoa, leo huku Mwenyeki wa CCM Mkoa wa Mwanza, Michael Masanja ‘Smart’ akiteta na Katibu wa Mkoa, Omar Mtuwa (kushoto).
Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza, Omar Mtuwa akizungumza wakati wa majumuisho ya ukaguzi wa  utekelezani wa ilani, leo wilayani Misungwi. (Picha zote na Baltazar Mashaka)
…….

NA BALTAZAR MASHAKA, MISUNGWI

UONGOZI wa Shule mpya ya Msingi Shilabela,wilayani Misungwi, umeipongeza serikali ya awamu ya sita kwa kuboresha sekta ya elimu ikiwemo kujenga miundombinu ya madarasa na matundu ya vyoo na kununua samani.

Pongezi hio imetolewa leo, na Mwalimu wa Taaluma wa shule hiyo, Modester Aloyce baada ya Kamati ya Siasa ya Mkoa wa Mwanza,kukagua ujenzi wa shule hiyo msingi Shilabela uliogharimu sh. milioni 540.3 kupitia mradi ya BOOST ukiwa ni utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM 2020-2025.

Amesema shule hiyo yenye wanafunzi 1,035 imejengwa na serikali mwaka 2022/23 ili kupunguza msongamano wa watoto katika Shule ya Msingi Mbela yenye wanafunzi 2,610 huku mundombinu ikiwa haikidhi mahitaji.

“Tunaipongeza Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dk. Samia Suluhu Hassan,kwa kuboresha sekta ya elimu ya msingi,ameleta fedha za kujenga jengo la utawala la shule ya Shilabela,ofisi 4 za walimu,madarasa 16,matundu 27 ya vyoo vya wanafunzi wa awali,msingi na walimu,”amesema. 

Naye Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mwanza,Michael Masanja ‘Smart’ kwa niaba ya Kamati ya siasa baada ya kukagua mradi huo wa BOOST amesema,Rais Dk.Samia na serikali yake amefanya kazi kubwa ya kuboresha elimu husasani ujenzi wa miundombinu na ununuzi wa samani.

“Zimeletwa fedha nyingi za uboreshaji wa elimu mkoani kwetu (Mwanza),zimetoka kwa Dk. Samia hivyo wanafunzi watambue kuwa Rais huyo wa Awamu ya Sita anawapenda na ameridhia kuwaletea fedha za kuboresha miundombinu ya elimu,haya tulizoea kuyaona shule binafsi leoe amebadilisha hali hiyo,”amesema.

Samrt amekiri madarasa hayo ya mradi wa BOOST yamejengwa kwa kiwango cha ubora na akatoa rai kwa wanafunzi kusoma kwa bidii wafaulu kwa kiwango cha juu kuifanya shule ya mfano pia,waitunze miundombinu hiyo idumu kwa kizazi cha ssa na vijavyo. 

Awali kamati hiyo ilikagua na kuridhishwa na mradi wa mabweni mawili ya wasichana Misungwi Sekondari yaliyogharimu sh.milioni 192 

“Niwapongeze kwa usimamizi mzuri wa fedha za miradi hii ya mabweni ya wasichana,rai yangu someni kwa bidii na kufaulu kwa daraja la kwanza,ukosefu wa umeme hilo litashughilikiwa watoto wasome hata usiku,”alisema Smart na kuahidi kuwapelekea Luninga wapate taarifa na kufahamu yanayofanywa na serikali yao.

Kwa mujibu wa Mkuu wa Shule hiyo, Alnold Rwiza bweni moja limekamilika kwa sh. milioni 62 litachukua wanafunzi 94 na jingine linalojengwa kwa sh. 129 wanatarajia kuchukua wanafunzi 194, lengo ni kuboresha mazingira ya kujifunza na kufundishia,changamoto ni kutounganishwa na nishati ya umeme.