HALMASHAURI ya Wilaya ya Nachingwea imeendelea kuwashangaza wengi kwa namna ilivyobeba Tuzo Lukuki za Elimu ngazi ya Mkoa wa Lindi zinazotokana na matokeo ya usimamizi na ufaulu wa mitihani mbalimbali ya kitaifa ya Mwaka 2023.
Akikabidhi Tuzo hizo,Mkuu wa Mkoa wa Lindi Zainab Telack wilayani Ruangwa alisema kuwa Halmashauri ya wilaya ya Nachingwea imepata tuzo za Shule bora ya kwanza ya kidato cha sita,Mwalimu bora ngazi ya mkoa, tuzo ya usimamiaji na ubora wa miradi ya elimu Nachingwea.
Telack alisema kuwa Mwanafunzi bora kidato cha sita kwa mkoa wa Lindi,shule ya mchepuo wa kiingereza ya Silver imetoa mwanafunzi bora,Afisa Elimu kata bora kutoka Mkoa wa Lindi na Bodi ya shule bora Mkoa wa Lindi ni Nachingwea Girls.
Aidha Mkuu wa mkoa wa Lindi Zainab Telack alisema kuwa Halmashauri iliyotoa fedha nyingi za mapato ya ndani katika kuboresha miundombinu ya Elimu ni Nachingwea,michezo sasa Nachingwea ni mshindi wa jumla kwenye michezo ya UMITASHUMTA na UMISSETA ngazi ya Mkoa na Halmashauri ya Nachingwea miongoni mwa zilizopata Tuzo vigezo vya KPI ufaulu zaidi ya 85%.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mhandishi Chionda na Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Adinani Mpyagila wanawashukuru na kuwapongeza wadau wote kwa ushirikiano na walisema kuwa wameshinda Tuzo zaidi ya 30.