Viongozi mbalimbali wa Serikali na Sekta Binafsi wakiwa kwenye Maadhimisho
ya Siku ya Wafanyakazi Duniani ambayo Kitaifa imefanyika katika Uwanja wa
Sheikh Amri Abeid Mkoani Arusha tarehe 01 Mei 2024.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip
Mpango akiwa na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa, Naibu Waziri Mkuu na
Waziri wa Nishati Dkt. Dotto Biteko, Spika wa Bunge Mhe. Dkt. Tulia Ackson,
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu)
Deogratius Ndejembi, Katibu Mkuu Kiongozi Mhe. Dkt. Moses Kusiluka, Rais
wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi nchini (TUCTA) Tumaini Nyamhokya,
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Paul Makonda pamoja na Viongozi wengine
wakiimba Wimbo wa Mshikamano (Solidarity) wakati wa Sherehe ya Mei Mosi
ambazo Kitaifa zimefanyika katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid Mkoani
Arusha tarehe 01 Mei 2024.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip
Mpango akihutubia Viongozi na Wafanyakazi kutoka Wizara, Taasisi za Serikali
na Binafsi wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani ambayo
Kitaifa yamefanyika katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid Mkoani Arusha
tarehe 01 Mei 2024.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip
Mpango akizindua Gazeti la Mfanyakazi Tanzania wakati wa Maadhimisho ya
Siku ya Wafanyakazi Duniani ambayo Kitaifa yamefanyika katika Uwanja wa
Sheikh Amri Abeid Mkoani Arusha tarehe 01 Mei 2024. Kushoto ni Waziri Mkuu
Mhe. Kassim Majaliwa na kulia ni Rais wa Shirikisho la Vyama vya
Wafanyakazi nchini (TUCTA) Tumaini Nyamhokya.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip
Mpango akionesha Gazeti la Mfanyakazi Tanzania mara baada ya kulizindua
wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani ambayo Kitaifa
yamefanyika katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid Mkoani Arusha tarehe 01
Mei 2024.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip
Mpango akitoa zawadi ya ujumla kwa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
ambao wameongoza katika michezo mbalimbali katika kuadhimisha ya Siku ya
Wafanyakazi Duniani ambayo Kitaifa imefanyika katika Uwanja wa Sheikh
Amri Abeid Mkoani Arusha tarehe 01 Mei 2024.
……………………
Happy Lazaro,Arusha .
Arusha .Makamu wa Rais ,Philip Mpango amesema kuwa, kuhusu sheria mbalimbali za mkataba wataendelea kufanya maboresho mbalimbali ili kuhakikisha wafanyakazi wanapata haki zao.
“Wafanyakazi wanaoajiriwa kupitia njia zote wanahitaji kupatiwa haki zote za msingi kama ilivyo kwenye ajira.”amesema .
“Tunashukuru sana kwa ushauri wenu ambao una maslahi mapana ya nchi yetu pamoja na kuboresha maslahi ya wafanyakazi kwa ujumla .”amesema .
“Serikali inatambua fursa ya vijana katika kupata mafunzo mbalimbali ambapo wanaendelea kujenga vyuo mbalimbali vya ufundi kwa lengo la kuwezesha vijana kupata ufundi na kuajirika zaidi.
Amesema kuwa,Serikali itaendelea kuboresha mazingira ya vitendea kazi mahala pa kazi.
“Ni lazima kufuata sheria na taratibu katika utumishi wa umma , na serikali itaendelea kuhakikisha eneo hilo linakuwa vizuri.”
Katika kuhakikisha wananchi wanapata bima ya afya serikali imefanya maboresho katika mfuko wa bima ya afya .
Aidha amewataka waajiri kuhakikisha wanawasilisha michango ya wafanyakazi wao kwa wakati .
Aidha amewataka wafanyabiashara kutumia fursa hiyo kulipa kodi kwa wakati ili kuweza kuboresha maslahi ya wafanyakazi,ambapo serikali inatambua umuhimu wa kupunguza ugumu wa maisha.
‘Kuhusu changamoto mlizosema hapa kama serikali tutalifanyia kazi kuhakikisha haki za wafanyakazi zinafanyiwa kazi
‘Endapo ugumu wa maisha utaendelea muda wowote Mh Samia Suluhu Hassan atasema neno kwa wafanyakazi nchini
“amesema Mpango.