Katibu wa TUCTA, Hery Mkunda amesema kuwa maboresho yaliyofanyika bado hayakidhi mahitaji ya wafanyakazi hivyo wameomba serikali waangalie swala hilo ili kuwezesha mfanyakazi kupata maslahi yao .
Amesema kuwa,siku ya wafanyakazi inatekeleza mambo mengi kwa maendeleo ya wafanyakazi lengo likiwa ni kuhakikisha wanakuwa na mazingira bora katika utendaji kazi .
Amesema kuwa,kauli mbiu ya mwaka huu ni ” nyongeza ya mshahara ni msingi wa mafao bora na kinga dhidi ya hali ngumu ya maisha .”
Amesema kuwa kauli mbiu hiyo inasaidia katika kupambana na hali ngumu ya maisha .
Hali ngumu ya maisha inasababisha kushindwa kumudu gharama za maisha na njia pekee ya kuondokana na changamoto ya maisha duni ni kuongezeka kwa mshahara.
“Hali ngumu ya maisha inasababisha na kupanda kwa gharama ya maisha kwa wafanyakazi kuongezeka kwa mfumo wa bei kunaambatana na kodi nyingi na kusababisha hali ngumu ya maisha kwa wafanyakazi.
Aidha amesema kuwa,anapendekeza watumishi wote walipwe haki zao sambamba na kuwepo kwa maboresho mbalimbali kwa wafanyakazi .
“Tucta inaendelea kutoa elimu zaidi kuhusu maswala ya bima ya afya kwa wananchi na wafanyakazi ili kuweza kujua manufaa yake na kuweza kuitumia kwa manufaa yao. “.
Aidha ameiomba serikali kuwapa likizo ya uzazi wafanyakazi wanaojifungua watoto Njiti ili wapate muda mrefu wa kulea mtoto huyo.
Naye Rais wa Tucta,amesema kuwa ni vizuri wafanyakazi wa kada wakaongeze elimu katika kada zao katika kada za afya na kilimo ili kuongeza ujuzi zaidi.