Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhandisi Amani Mafuru akifungua mafunzo ya utoaji wa barua za utambulisho kupitia mfumo wa kidijitali wenye kanzidata ya anuani za makazi (NaPA) yaliyotolewa kwa wenyeviti wa mitaa, watendaji wa mtaa, watendaji wa kata, waratibu wa anuani za makazi wa halmashauri na mratibu wa mkoa wa Dar es Salaam.
Washiriki wa mafunzo ya utoaji wa barua za utambulisho kupitia mfumo wa kidijitali wenye kanzidata ya anuani za makazi (NaPA) wakimsiliza Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhandisi Amani Mafuru (hayupo pichani) wakati akifungua mafunzo hayo jiji Dar es Salaam katika ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa.
Mhandisi wa Mifumo wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia Bw. Medson Naftali akitoa mafunzo ya utoaji wa barua za utambulisho kupitia mfumo wa kidijitali wenye kanzidata ya anuani za makazi (NaPA) kwa wenyeviti wa mitaa, watendaji wa mtaa, watendaji wa kata, waratibu wa anuani za makazi wa halmashauri na mratibu wa anuani za makazi mkoani Dar es Salaam.
Mhandisi wa Mifumo wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia Bw. Medson Naftali akisikiliza kwa makini maswali ya washiriki wa mafunzo ya utoaji wa barua za utambulisho kupitia mfumo wa kidijitali wenye kanzidata ya anuani za makazi (NaPA) yaliyofanyika jijini Dar es Salaam katika Ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa.
Mhandisi wa Mifumo wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia Bw. Medson Naftali akijibu maswali yaliyoulizwa na washiriki wa mafunzo ya utoaji wa barua za utambulisho kupitia mfumo wa kidijitali wenye kanzidata ya anuani za makazi (NaPA), mara baada ya kutoa mafunzo hayo jijini Dar es Salaam katika Ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa.
Mshiriki wa mafunzo ya utoaji wa barua za utambulisho kupitia mfumo wa kidijitali wenye kanzidata ya anuani za makazi (NaPA) Bi. Khadija Athumani akieleza faida za mafunzo hayo waliyopatiwa na Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais-TAMISEMI.
Mshiriki wa mafunzo ya utoaji wa barua za utambulisho kupitia mfumo wa kidijitali wenye kanzidata ya anuani za makazi (NaPA), Bi. Rozina Kimario akieleza faida za mafunzo hayo waliyopatiwa na Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais-TAMISEMI.
………….
Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhandisi Amani Mafuru amesema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amedhamiria anuani za makazi zirahisishe utoaji wa huduma kwa wananchi kwa njia ya kidijitali.
Amesema hayo jijini Dar es Salaam, wakati akifungua mafunzo ya utoaji wa barua za utambulisho kupitia mfumo wa kidijitali wenye kanzidata ya anuani za makazi (NaPA) yaliyotolewa kwa wenyeviti wa mitaa, watendaji wa mtaa, watendaji wa kata, waratibu wa anuani za makazi wa halmashauri na mratibu wa mkoa wa Dar es Salaam.
Mhandisi Mafuru amehimiza kuwa, Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais-TAMISEMI imetoa nafasi ya kipekee kwa halmashauri za mkoa wa Dar es Salaam kufanya zoezi la majaribio ya kutoa barua za utambulisho kidijitali na ndio maana inatoa mafunzo ya kuwajengea uwezo watendaji wanaotoa huduma hiyo.
“Azma ya Mheshimiwa Rais ni kuona Mfumo wa Anuani za Makazi unarahisha utoaji wa huduma ya barua ya utambulisho wa wananchi kidijitali,” Mhandisi Mafuru amesisitiza.
Naye, mshiriki wa mafunzo hayo Bi. Khadija Athumani ambaye ni Afisa Mtendaji wa Mtaa wa Amana Kata ya Ilala amesema kuwa, anaishukuru Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia pamoja na Ofisi ya Rais-TAMISEMI kwa kuwapatia mafunzo yatayowarahishia utoaji wa barua ya utambulisho kidijitali hivyo kurahisisha utendaji kazi wao.
Kwa upande wake, Bi. Rozina Kimario ambaye ni Afisa Mtendaji wa Kata ya Manzese, Manispaa ya Ubungo amesema, wameyapokea mafunzo vizuri kwani barua za utambulisho watakazozitoa kidijitali zitawaondolea wananchi usumbufu kwani watapatiwa huduma hiyo popote walipo bila kulazimika kwenda kwenye ofisi ya mtendaji wa mtaa au kata.