NJOMBE
Ikiwa siku 10 zimepita tangu chama cha demokrasia na maendeo chadema kifungue dirisha kwa ajili ya watia nia wa uongozi wa chama hicho mkoa Njombe kuchyukua fomu za kuwania nafasi mbalimbali ,Ahadi Asajile Mtweve mwandishi wa habari wa kujitegemea mstaafu amechukua fomu ya kugombea nafasi ya mwenyekiti wa chadema mkoa huku malengo yake makubwa kukifanya chama kupata ushindi mkubwa katika uchaguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu wa Rasi ,Wabunge na Madiwani.Mtia Nia huyo amesema amefikia uamuzi wa kugombea nafasi hiyo baada ya kufanya kazi za chama kwa muda mrefu katika ngazi ya jimbo na kanda kwa mafanikio makubwa na kisha kuwa ahidi wafuasi wa chadema Njombe na wilaya zake kuimarisha umoja na mshikamano ili kutokomeza makundi ambayo yamekuwa yakitokeza kutokana na makovu ya chaguzi huku pia akisema katiba ndiyo utakuwa muongozo wake kuelekea nchi ya ahadi.Awali akizungumzia zoezi hilo Baraka Kivambe Katibu wa chama cha demokrasia na maendeleo chadema Njombe amesema mwamkoa umekuwa mkubwa kwa watia nia kuchukua fomu za kugombea nafasi mbalimbali za uongozi tangu dirisha la kuchukua fomu lifunguliwe marchi 11 na kutarajiwa kufungwa leo machi 21 jambo ambalo ni kiashiria tosha cha kukua kwa demokrasia ndani ya chama hicho .

Kivambe amesema watia nia ambao wameshachukua fomu hadi sasa Ahadi Asajile Mtweve mgombea wa nafasi ya mwenyekiti mkoa ,Ebron Mwakyegula mgombea uwenyekiti baraza la wazee huku akiwataja wengine waliyochukua fomu kuwa ni Veronica Mlonganile anaegombea nafasi ya mwenyekiti wa baraza la wanawake BAWACHA na Fomu ya mgombea wa nafasi ya katibu wa baraza la wanawake BAWACHA Msifuni Mahenge ambao wote wawili wameshazirejesha baada ya kuzijaza.

“Sifa za kiongozi tunaemtaka awe na hamu ya kuona CCM wanaondoka madarakani ,Kiongozi muwajibikaji na mpambanaji usiku na mchana kwa maslahi ya chama hivyo tunategemea uchaguzi huu utakwenda kutupa viongozi tunao wataka,alisema Kivambe “

Kwa upande wake Ebron Mwakyegula mtia nia wa nafasi ya mwenyekiti baraza la wazee anasema amegombea amechukua fomu kuitaka nafasi hiyo ili kupigania haki za wazee kwenye matibabu na huduma nyingine za kijamii na kisha kuhamasisha wazee wengine katika jamii kujiunga na chadema.

“Sisi Wazee tumetumikia taifa hili kwa muda mrefu lakini sasa hatuna nguvu za kutosha tunahitaji huduma za kijamii bure hivyo nikiaminiwa katika nafasi hii nitakwenda kupigania haki za wazee,alisema Ebron Kyegula mtia nia wa baraza la wazee chadema Njombe”

Miongoni mwa watia nia wengine waliorejesha fomu ikiwa saa chache zimesalia dirisha kufungwa ni pamoja na Msifuni Mahenge anaeitaka nafasi ya katibu wa BAWACHA Mkoa wa Njombe anaebebwa na agenda ya uwajibikaji katika utawala wake.