…………………..
Na Mwandishi wetu
Ruvuma
Wakazi wa Manispaa ya Songea,wamejitokeza kuuaga mwili wa aliyekuwa Meneja wa wakala wa Barabara( Tanroads )Mkoa wa Ruvuma Mhandisi Mlima Felix Ngaile( 55) aliyefariki ghafla juzi.
Marehemu Felix Ngaile ,alipatwa na mshituko wa moyo wakati akikikimbia Mbio za hisani za km 5 zilizoandaliwa na Shirika lilisilo la kiserikali la Wiloles Foundation kwa ajili ya kuchagia fedha za kununua vifaa tiba ili kuokoa maisha ya watoto waliozaliwa kabla ya muda (Njiti)
Akiongoza waombolezaji walijitokeza kwa wingi kwenye ibada iliyofanyika kanisa katoriki jimbo kuu la songea,Mkuu wa Wilaya ya Songea Wilman Kapenjama Ndile aliyemwakilisha mkuu wa Mkoa wa Ruvuma,Kanali Laban Thomas alisema,Marehemu amefariki kutokana na mshituko wa moyo (BP) .
Mkuu wa Wilaya Kapenjama Ndile alisema, kwamba pamoja na dhamila yake kubwa ya kuchangia watoto Njiti wa mkoa wa Ruvuma , alipatwa na mauti wakati akitimiza adhima ya kuhakikisha anashiriki mbio za hisani kama alivyokuwa ameahidi kwa waandaaji .
“kifo kinaukatili sana,kwasababu namna kinavyoondoa ndugu zetu wapo wanaoondoka ghafla kama mhandisi Ngaile , na wapo wanaougua na kulazwa hospitali na kuzidi kupoteza matumaini na baadaye taarifa za kifo zinapotokea tunasema ameteseka sana acha apumzike, hatusemi kifo kama hicho hakiuzunishi , tofauti na hiki kinachotokea ghafla kinaumiza zaidi ,”alisema Mkuu huyo wa Wilaya Kapenjama Ndile.
Aidha ,amewataka wananchi kuacha maneno kuwa Kuna hujuma imefanyika bali Mungu pekee ndiye anayejua na wauchukulie msiba huo kuwa ni wa kawaida
Wapo watakufa wakiwa safarini, kazini ,nyumbani ,hospitali na hata nyumba za wageni .
Pia Ibanda hiyo imehudhriwa na viongozi mbali mbali wa Chama na serikali , wananchi wakandarasi,watumishi wa taasisa na idara za serikali wakiwemo watumishi wa Tanroads mkoa wa Ruvuma wakiongozwa na mkuu wa kitengo cha matengenezo Mhandisi Roman Mbukwini.
Akiongoza Ibada hiyo Paroko wa jimbo kuu Songea Padri Daniel Oteno, amewataka waumini kutambua kuwa maisha ni mtihani,hivyo wanapaswa kujiandaa na endepo Mhandisi Felix angejua kuwa kwenye mazoezi yake ndio ingekuwa mwisho wake angewaaga marafiki zake kuwa hatorudi lakini tutambue maisha ni kama maua asubuhi yana chanua jioni yananyaukaa.
Padre Oteno, amewataka watumishi kwenye nafasi zao kufanya kazi kwa bidii ikiwa ni pamoja na kujenga tabia ya kumtegemea Mungu kwenye kila kitu wanachofanya ikiwa ni pamoja na kusali zaidi ili kujiandaa kwani Maisha ni mtihani tujiandae ,na kwamba Wafanyakazi wachukue kazi zao kama daraja la kwenda Mbinguni na siyo kutumia kazi zao kama mwisho wao na ,wafanye kazi zao kwa kutengeneza barabara kwa ajili utukufu wa kwenda mbinguni.
” kila mmoja kwa nafasi yake asijisahau katika msiba huu wa felix tuwe na sara , sara ya kwanza ya Yesu Ee bwana Mikononi mwako naiweka Roho yangu , hakuna zawadi sasa hivi kwa Felix kama sara hii , haya ni maneno ya Mbinguni ya utukufu , na kwa wale wote mtakao safiri kwenda Shinyanga sara hii msiiache “Alisema Padri Otieno.
Akisoma wasifu wa Marehemu Meneja wa Tanroads Mkoa wa Songwe ,Suleiman Bishanga ambaye aliwawakilisha Mameneja wa Tanroads nchini alisema, marehemu Ngaile alizaliwa Novemba 9,1968 amebahatika kufanya kazi katika mikoa mbali mbali ikiwemo Mwanza, Mara, kilimanjaro na hadi anapatwa mauti alikuwa ni Meneja wa Mkoa wa Ruvuma ambapo alilipoti Oktoba 2023 na ameacha mjane na watoto watatu , atakumbukwa kwa uhodari wake na pengo lake ni gumu kuzibika. .
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Wakandarasi Mkoa wa Ruvuma, Charles Mhagama amesema amepokea kifo hicho kwa uchungu mkubwa wanamuachia Mungu kwani alikuwa msaada kwa wakandarasi na alitatua kero zao kwa wakati muhafaka.
“Kifo Sawa na mtego ni vema kucheki afya mara kwa mara na tutende mema kama ambavyo marehemu alikuwa akifanya ili hata muda wa kuondoka duniani ukifika tukumbukwe kwa mema kama Mhandisi Ngaile,”alisema Mhagama.
Mhandisi Roman Mbukwini Msimamizi wa kitengo cha Matengenezo wa wakala wa barabara(Tanroads)mkoa wa Ruvuma Mhandisi Roman Mbukwini alisema,kiongozi ambaye alikuwa kama Baba kwa watumishi wa chini yake kwani alipenda sana kuwashirikisha na kuwafundisha kazi.
“Alikuwa ni zaidi ya mwalimu, zaidi ya baba na kiongozi kwa watumishi wenzake”
Aidha Mbukwini,amewashauri wati wanapoandaa mashindano ya riadha yanayowashirikisha watu wa rika na umri tofauti ni vema kwanza wawapime watu afya zao kabla ya kuanza mashindano ili kuepuka matatizo yanayoweza kutokea.