Ashrack Miraji Same Kilimanjaro
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi CCM Wilaya ya SAME Cde.Azza Karisha amehitimisha mashindano ya SAMIA CUP yaliyokuwa yanachezwa kwenye Tarafa ya Mamba Vunta, Jimbo la Same Mashariki michezo iliyo andaliwa na Mbunge wa Jimbo Hilo mhe.Anne Kilango.
Mashindano hayo yamehitimishwa kwa mchezo wa Fainali uliokutanisha timu za Nyuki FC kutoka Kata ya Vunta na Zimbwe FC kutoka kata ya Mpinji amapo timu ya Zimbwe FC iliibuka mshindi kwenye fainali hiyo na kutangazwa kuwa Mabingwa wapya.
Pamoja na mambo Mengine Mwenyekiti huyo wa UVCCM amemshukuru Mbunge wa Jimbo la Same Mashariki Mhe. Anne Kilango kwa kuamua Kuanzisha Mashindano ikiwa ni Sehemu ya Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi CCM akisema Mashindano hayo yamekuwa na tija kubwa kwa Vijana kwa maana ya Kujenga umoja, Upendo, mshikamano Lakini pia na kuimarisha afya zao.
“Niendelee Kumshukuru na Kumpongeza Mwenyekiti wetu was chama Taifa ambae ndie Rais wetu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassani na serikali yake kwa namna ambavyo amewajali Wananchi wa Tarafa ya Mamba Vunta na Kuwaletea Fedha Nyingi za Maendeleo kwenye sekta Mbalimbali ikiwepo Elimu, afya, barabara, kilimo nk”. Alisema Mwenyekiti huyo wa UVCCM wiaya ya Same.
Pamoja na hayo amewaomba wananchi wa Mamba Vunta kuendelea kumuunga Mkono Mhe.Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan na Mbuge wa jimbo la Same Mashariki Anne Kilango na chama Cha Mapinduzi kwani ndicho akisema ndio chama pekee kinachoweza Kuwaletea Wananchi Maendeleo.
Aidha katika hatua nyingine mwenyekiti huyo aliongoza zoezi la upandaji Miti kwenye shule ya Msingi Mpinji mwendelezo wa utekelezaji wa kampeni ya Utunzaji wa Mazingira na kuifanya Same iwe ya kijani.
Katibu wa Mbunge wa jimbo la Same Mashariki Semu Mmamba Amesema jimbo la Same Mashariki lina tarafa tatu tarafa Moja wamemaliza mashindano hayo bado tarafa mbili kila tarafa inapaswa kutoa mshindi wa kwanza mpaka watatu hili kupata Timu 9 ambazo zitaunda Tena mashindo ya Samia Cup washindi wa tatu wanaopatikana kwa kila tarafa watapatiwa zawadi baada ya mashindano hayo kukamilika na kumpata mshindi wa jimbo wa ligi ya SAMIA CUP.