Kamishna wa Idara ya Uchambuzi wa Sera, Wizara ya Fedha, Bw. William Mhoja, akieleza kuhusu umuhimu na mchango wa sekta binafsu katika kukuza uchumi wakati wa Kongamano la Jukwaa la Wafanyabiashara Mkoa wa Shinyanga ambapo Wizara ya Fedha ilitumia fursa hiyo kukusanya maoni ili kuweza kuboreshaji utozaji Kodi kwa mwaka 2024/25.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Dkt. Hashil Abdallah (kulia) na Kamishna wa Idara ya Uchambuzi wa Sera, Wizara ya Fedha, Bw. William Mhoja, wakisikiliza maoni ya wananchi kuhusu maboresho ya utozaji Kodi, wakati wa Kongamano la Jukwaa la Wafanyabiashara lililoandaliwa na Mkoa wa Shinyanga.
Meneja wa Usajili wa Malalamiko ya Kodi kutoka Taasisi ya Usuluhishi wa Malalamiko na Taarifa za Kodi (TOST), Bi. Naomi Mwaipola, akiwataka wafanyabiashara wa Mkoa wa Shinyanga kuitumia taasisi hiyo wanapokuwa na malalamiko mbalimbali ya kikodi ili kuweza kuyapatia ufumbuzi bila kuegemea upande wowote, wakati wa Kongamano la Jukwaa la Wafanyabiashara liliofanyika Mkoni Shinyanga.
Mwenyekiti Chama cha Wafanyabiashara, Viwanda na Kilimo (TCCIA) mkoa wa Shinyanga, Bw. Jonathan Manyama, akieleza utayari wa wafanyabiashara kulipa kodi na pia akaiomba Serikali kufanyia kazi maoni ya Wafanyabiashara hao kuhusu kodi, wakati wa Kongamano la Jukwaa la Wafanyabiashara liliofanyika Mkoni Shinyanga
Mkurugenzi wa Hotel ya Karina ya Mkoani Shinyanga, Bi. Josephine Wambura, akiomba ufafanuzi kuhusu Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT), wakati wa Kongamano la Jukwaa la Wafanyabiashara liliofanyika Mkoni Shinyanga, ambapo Wizara ya Fedha ilitumia fursa hiyo kukusanya maoni ili kuweza kuboreshaji utozaji Kodi kwa mwaka 2024/25.
Kamishna wa Idara ya Uchambuzi wa Sera, Wizara ya Fedha, Bw. William Mhoja (kushoto) akiteta jambona Mwenyekiti Chama cha Wafanyabiashara, Viwanda na Kilimo (TCCIA) mkoa wa Mbeya, kabla ya kuanza kwa Kongamano la Jukwaa la Wafanyabiashara liliofanyika mkoani Shinyanga, ambapo Wizara ya Fedha ilitumia fursa hiyo kukusanya maoni ili kuboreshaji utozaji Kodi kwa mwaka 2024/25.
Mkurugenzi wa Kiwanda Kidogo cha Kutengeneza kinywaji cha Furaha Tangawizi mkoani Shinyanga, akitoa maoni kuhusu uboreshaji wa utozaji kodi, wakati wa Kongamano la Jukwaa la Wafanyabiashara liliofanyika Mkoni Shinyanga, ambapo Wizara ya Fedha ilitumia fursa hiyo kukusanya maoni ili kuboreshaji utozaji Kodi kwa mwaka 2024/25.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Dkt. Hashil Abdallah (katikati) na Kamishna wa Idara ya Uchambuzi wa Sera, Wizara ya Fedha, Bw. William Mhoja, (wa tatu kulia) wakiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa Wafanya biashara Mkoa wa Shinyanga na Mbeya, pamoja na wadau wengine kabla ya Kongamano la Jukwaa la Wafanyabiashara lililoandaliwa na Mkoa wa Shinyanga.
…………………………..
mchango wa Sekta Binafsi katika uwekezaji hivyo imeendelea kuboresha mazingira ya uwekezaji na biashara ili iweze kukuza uchumi wa nchi.
Alisema kuwa Serikali inaendelea kuimarisha miundombinu wezeshi ya usafirishaji na Nishati, kuhakikisha uhimilivu wa viashiria vya uchumi jumla na kuwa na sera za kodi zinazotabirika na kuwianisha tozo na ada mbalimbali zinazotozwa na Wizara na Mamlaka za Udhibiti.
Naye Meneja wa Usajili wa Malalamiko ya Kodi wa Taasisi ya Usuluhishi wa Malalamiko na Taarifa za Kodi (TOST), Bi. Naomi Mwaipola, aliwataka wafanyabiashara na wadau waitumie taasisi hiyo ambayo inajitegemea kwa kuleta malalamiko ya kikodi ili kuweka mazingira ya haki na usawa.
“Unapoona hujatendewa haki unatakiwa kufika kwenye taasisi yetu bila kutozwa gharama tofauti tofauti na unapotumia Mahakama, lengo ni kumfanya mlipa kodi asiwe na manung’uniko yoyote” alisema Bi. Mwaipola.
Naye Mwenyekiti Chama cha Wafanyabiashara, Viwanda na Kilimo (TCCIA) Mkoa wa Shinyanga, Bw. Jonathan Manyama, ameiomba Serikali kuwa na uwazi katika utozaji kodi ili wafanyabiashara wajue kama kodi hizo zinafika eneo lilokusudiwa.
Amesema Wafanyabiashara wataendelea kulipa kodi kwa kuwa wanatambua kuwa ndio chanzo cha uboreshaji wa sekta mbalimbali zikiwemo za afya, miundombinu ya barabara, elimu na nishati.
Timu ya Wataalam wa Uchambuzi wa Sera za Kodi kutoka Wizara ya Fedha imeendelea na ukusanyaji wa maoni kwa wananchi Kikanda ili kuboresha Sera ya utozaji kodi kwa mwaka wa Fedha 2024/25, ambapo mikoa wa Arusha, Mwanza na Shinyaka imefikiwa.