Na Catherine Kuchaka – Dodoma
Naibu Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Hamis Mwinjuma ameipongeza Timu ya 77 MTUMBA FC kwa kuibuka Mshindi wa NDONDO CUP 2023 baada ya kuifunga GWASSA FC kwa mikwaju minne ya Penati katika mchezo uliochezwa Novemba 10, 2023 Uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma .
Mhe.Mwinjuma ameridhishwa na mashindano hayo ambayo yapo chini ya Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini na Waziri wa Madini Mhe. Anthony Mavunde akieleza kuwa yamekuwa chachu ya kuibua na kuendeleza vipaji.
“Mashindano ya ndondo yanahamisha jamii kushiriki katika michezo na yanaunga mkono juhudi za Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan pamoja na wadau kutoka Sekta binafsi kuendeleza michezo, sisi kama Wizara tunaweka mkazo katika maendeleo ya michezo yote hapa nchini”.
Kwa upande wake Mhe. Anthony Mavunde emeeleza kuwa lengo la mashindano hayo ni kusaidia kukuza vipaji vya vijana wa mtaani kuonekana na kuwasimamia, ambapo ameahidi kuendelea kuwaunga mkono vijana waliofanya vizuri katika mashindano hayo ikiwemo kuwatafutia timu za kucheza.