Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Albert Charamila anatarajiwa kuungana na wakazi wengine 400 wa jijini humo kwa ajili ya kushiriki mbio za hisani zilizoandaliwa na Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) zitakazofanyika Oktoba 29 katika viwanja vya Mlimani City.
Mbio hizo za hisani ni sehemu ya muendelezo wa matukio ya kusherehekea miaka 20 ya taasisi hiyo ambayo tangu ilipoanzishwa mwaka 2003 mpaka sasa inaonekana kupiga hatua kubwa na kujiimarisha katika nyanja mbalimbali.
Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es salaam mapema Octoba 26 kuhusiana na mbio hizo Mwenyekiti wa maandalizi ya Maadhimisho hayo Mellania Kasese amesema lengo la shughuli hiyo ni kutunisha mfuko wa upandaji miti katika maeneo kame na kampeni za upandaji mito
“Mbio hizo zitakuwa za km tano na kumi,maandalizi yameshakamilika vifaa vyote vimeshafika na mpaka sasa tunavyoongea tiketi zote 400 ambazo zilitengwa kuuza kwa ajili ua washiriki zimeshaisha siku tatu nyuma,”alisema Kasese.
Naye katibu wa Chama Cha Riadhaa Mkoa wa Dar es salaam , Samweli Mwela ambao ndiyo wasimamizi wa mbio hizo amesema tangu awali wamekuwa wakishirikiana na TCAA katika maandalizi ya mbio hizo wamekuwa walishirikiana vyema katika maandalizi kutokana na Chama hicho ndio limekuwa kikiusika katika mbio zote.
“Tumejiridhisha na tumehakikisha njia zitakazotumika kwanza zimepimwa na salama,tunasubiri Jumapili kwa ajili yakuhitimisha tukio lenyewe,”amesema Mwela.
Aidha ametoa wito kwa wadau wengine wanaofanya mbio za hisani kushirikiana na Chama hicho Ili kuweza kuepukana na chagamoto mbalimbali ambazo zinaweza kujitokeza.
“Kumekuwa na changamoto kwa watu wengine kutohusisha chama cha riadha wanapoandaa mbio ni hatari sana ukipata jambo utakuwa hauna pakupeleka kama hivi wamefanya jqmbo la kuhimu na kuweza kujua nini chakufanya,”amesema Mwela.