Waziri wa Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa (wa pili kulia) akiwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Reli Tanzania (TRC), Ally Amani (wa pili kushoto), Mkurugenzi wa Huduma za Kimenejimenti, Ofisi ya Msajili wa Hazina, Neema Musomba (kulia) na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TRC, Amina Lumuli wakikata utepe kuashiria uzinduzi wa bodi ya TRC, jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa akisisitiza jambo kwa Mwenyekiti na Wajumbe wa Bodi ya Shirika la Reli Tanzania (TRC) hawapo pichani wakati alipozindua bodi hiyo, jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu Wizara ya Uchukuzi, Prof. Godius Kahyarara akisisitiza jambo kwa Mwenyekiti na Wajumbe wa Bodi ya Shirika la Reli Tanzania (TRC) hawapo pichani kabla bodi hiyo kuzinduliwa na Waziri wa Uchukuzi, Prof Makame Mbarawa jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Huduma za Kimenejimenti, Ofisi ya Msajili wa Hazina, Neema Musomba akizungumza na Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Reli Tanzania (TRC) Hawapo pichani wakati wa uzinduzi wa Bodi hiyo, jijini Dar es Salaam.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), Amina Lumuli, akitoa taarifa ya Utendaji wa shirika hilo wakati wa Uzinduzi wa bodi hiyo uliofanywa na Waziri wa Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa, jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi hiyo Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Reli Tanzania (TRC), Ally Amani.
Waziri wa Uchukuzi, Pro. Makame Mbarawa akitoa maelekezo kwa Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Prof. Godius Kahyarara mara baada ya Waziri huyo kuzindua bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Uchukuzi, Pro. Makame Mbarawa akimsikiliza Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Reli Tanzania (TRC) Ally Amani mara baada ya Waziri huyo kuzindua bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), jijini Dar es Salaam.
Sehemu ya Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Reli Tanzania (TRC) wakimsikiliza Waziri wa Uchukuzi, Pro. Makame Mbarawa (hawapo pichani), wakati alipozindua bodi ya TRC, jijini Dar es Salaam.
………….
Waziri wa Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa ameitaka Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Reli Tanzania (TRC) kuhakikisha inaisimamia Menejimenti kwenye eneo la uendeshaji ili kuboresha utoaji wa huduma hususani kwa wasafirishaji wa mizigo.
Akizungumza jijini Dar es Salaam wakati akizindua bodi hiyo Waziri Prof. Mbarawa amesema ufanisi katika huduma za reli utaongeza mzigo na kulifanya shirika hilo kuweza kujiendesha kwa faida.
“Kwenye eneo la ujenzi mnakwenda vizuri lakini bado kwenye uendeshaji hakuna utendaji mzuri, leo wasafirishaji wana mzigo wa kutosha lakini wakija kutafuta mabehewa wanaambiwa wakae foleni, hii haiwezekani kuendelea namna hii, Mwenyekiti simamia hili’ amesema Waziri Prof. Mbarawa.
Waziri Prof. Mbarawa ameeleza umuhimu wa matumizi ya tiketi mtandao kwa abiria na kuitaka TRC kuboresha mifumo ili kupunguza usumbufu unaojitokeza kwa abiria wanaolazimika kukaa muda mrefu kusubiria kukata tiketi wanapotaka kusafiri.
Aidha, Waziri Mbarawa ameongeza kuwa lengo la Serikali ni kuhakikisha reli zote mbili zinakuwa na tija hivyo ameitaka TRC kuchukua hatua stahiki kwa kutafuta wabia watakaoendesha treni maraa baada ya ujenzi na ukarabati kukamilika.
Naye Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Prof. Godius Kahyarara amesema Serikali itaendelea kuhakikisha fedha inazotenga kwenye bajeti za kila mwaka zinatumika katika kuboresha shirika hilo ambalo bado linahitaji vitendea kazi ili kujiendesha.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi hiyo Ally Amani amemuhakikishia Waziri Prof. Mbarawa kuwa Bodi imejipanga kutumia uzoefu ulionao kuhakikisha shirika hilo linakuwa na tija na kujiendesha kwa faida.(Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Uchukuzi)