Balozi wa Norway nchini Tanzania na Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mitaji na Maendeleo (UNFCC) Bw. Peter Malika wakisaini makubaliano ya kushirikiana ya kiasi cha shilingi bilioni 7.3 kwa ajili ya kusaidia katika wilaya za Mkoa wa Dodoma katika kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi..
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo akizungumza wakati wa hafla ya kusaini makubaliano ya ushirikiano kati ya Serikali ya Tanzania na Norway kuhusu ushirikiano katika hifadhi ya mazingira jijini Dar es Salaam leo Septemba 07, 2023. Kushoto ni Waziri anayeshughulikia masuala ya Ushirikiano wa Maendeleo ya Kimataifa na nchi za Nordic Mhe. Anne Beathe Tvinnereim.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo na Waziri anayeshughulikia masuala ya Ushirikiano wa Maendeleo ya Kimataifa na nchi za Nordic Mhe. Anne Beathe Tvinnereim wakisaini makubaliano ya ushirikiani kati ya Serikali ya Tanzania na Norway kuhusu ushirikiano katika hifadhi ya mazingira jijini Dar es Salaam leo Septemba 07, 2023. Aneyeshuhudia ni Mkurugenzi wa Kitengo cha Huduma za Sheria Ofisi ya Makamu wa Rais Bw. Dustan Shimbo.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo na Waziri anayeshughulikia masuala ya Ushirikiano wa Maendeleo ya Kimataifa na nchi za Nordic Mhe. Anne Beathe Tvinnereim wakionesha nyaraka za makubaliano kati ya Serikali ya Tanzania na Norway kuhusu ushirikiano katika hifadhi ya mazingira jijini Dar es Salaam leo Septemba 07, 2023.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo na Waziri anayeshughulikia masuala ya Ushirikiano wa Maendeleo ya Kimataifa na nchi za Nordic Mhe. Anne Beathe Tvinnereim wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali mara baada ya hafla ya kusaini makubaliano ya ushirikiano kati ya Serikali ya Tanzania na Norway kuhusu ushirikiano katika hifadhi ya mazingira jijini Dar es Salaam leo Septemba 07, 2023.
.………………………
Na Sophia Kingimali
Ubarozi wa Norway nchini umetoa kiasi Cha bilioni 7.4 ili kuwezesha serikali kukabiliana na mabadiliko ya Tabia nchi.
Akizungumza baada ya kusaini mkataba wa ushirikiano (MoU) waziri() Suleiman Jafo amesema mabadiliko ya Tabia nchi yanachangia Kwa kiasi kubwa katika mafanikio ya binadamu lakini pia ni chachu Katika kufanikisha agenda 2030 ya malengo ya maendeleo endelevu.
“Makubaliano haya ni Moja Kati ya makubaliano yaliyofanywa na serikali ya Norway na serikali ya Tanzania katika mashirikiano ya kusimamia mabadiliko ya Tabia nchi”amesema Jafo
Amesema mabadiliko ya Hali ya hewa yameanza kuonyesha matokeo hasi kupitia mpango wa mazingira wa serikali wa mwaka 2022 mpaka 2931.
Amesema pesa hizo walizopatiwa zitaenda kutekeleza mikakati madhubuti itakayowezesha serikali za mitaa kujenga uwezo kupanga bajeti na kusimamia maswala yote yanayohusu mabadiliko ya Tabia nchi.
Kwa upande wake waziri wa ushirikiano wa kimataifa wa Norway Anne Tvinnereim amesema wataendeleza ushirikiano na Tanzania ili kuhakikisha mabadiliko ya Tabia nchi hayaathiri uzalishaji wa chakula Wala kuharibu miundombinu.
Nae Barozi wa Norway nchini umetoa Tonne Tinnes amesema serikali inathamini mchango wa kuwaleta pamoja washirika mbalimbali wa maendeleo ili kusaidia mabadiliko ya tabia nchi..
Kwa upande wake mkuu wa shirika umoja wa mataifa la mitaji ya maendeleo ( UNCDF)Peter Malika amesema ushirikiano na ubarozi wa Norway ni Mpya hivyo wanaamini utasaidia kuendeleza miradi mbalimbali inayoendelea nchini.
Amesema UNCDF kupitia mradi wa LOCAL unatoa ruzuku inayotokana na utendaji pamoja na msaada wa kiufundi ili kuweza kusaidia serikali kukabiliana na changamoto za mabadiliko ya Tabia nchi katika ngazi ya jamii.
“Tunaendelea kushukuru mashirikiano haya baina ya serikali ya Norway na serikali ya kupitia ofisi ya makamu wa rais idara ya mazingira na washirika wote wa maendele Kwa kuendelea kuwezesha shirika kufanikisha vipaumbele vya kukabiliana na mabadiliko ya Tabia nchi”amesema Malika
Fedha hizo zilizotolewa zitaenda kuendeleza miradi katika wilaya ya Chamwino,Kondoa na Mpwapwa lakini pia kuanzisha miradi katika wilaya nyingine tatu huku lengo likiwa kuzifikia wilaya zote nchini