……………….
Na Sixmund Begashe
Wakazi wa waishio jirani na Hifadhi ya Taifa Milima Udzungwa Wilaya ya Kilombero wameishukuru Serikali kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii Kwa kuboresha usalama wao Kwa kudhibiti Wanyama wakali na Waharibifu pamoja na Maboresho ya Hifadhi hiyo jambo linalowavutia Watalii wengi Hifadhini hapo.
Makazi wa Mang’ula Bw. Josephat Mwenda, amesema kuwa, kwa Sasa wananufaika na Hifadhi hiyo kupitia wageni wanaomiminika kwenye eneo hilo, pamoja na kupata elimu kuhusu umuhimu wa Utalii wa ndani na Uhifadhi kwa Gari la Sinema.
Naye Mhifadhi mwandamizi Hifadhi ya Taifa Milima Udzungwa ambaye pia ni Msimamizi wa Mradi wa Kukuza na Kuendeleza Utalii Kusini mwa Tanzania (REGROW) Joel Mrema ameeleza kuwa, kupitia Mradi umewezesha Magari, Vifaa mbalimbali, vinavyopelekea jamii na Watalii kunufaika na Hifadhi hiyo na muda si mrefu ujenzi wa Njia ya Juu ya Miti ndefu kuliko zote Afrika,Kwa ajili ya Watalii Utaanza.
Akiwa mwenye furaha kubwa ndani ya Hifadhi ya Udzungwa, Mtalii kutoka Hispani Bw. Carlos Madrigal ameupongeza Uongozi wa Hifadhi hiyo Kwa kuweka miundombinu rafiki pamoja na usalama wa uhakika Kwa Mtalii awapo ndani ya Hifadhi hiyo yenye Maporomoko ya Maji marefu na yenye kuvutia.